Yusuf Abdulazeez (alizaliwa 9 Machi 2002) ni mchezaji mahiri wa soka kutoka Nigeria anayeshiriki kama mshambuliaji katika timu ya Mjällby AIF katika ligi ya Allsvenskan.

Kazi ya Soka hariri

Abdulazeez alianza kucheza katika timu ya ndani katika mji wake wa Akure kabla ya kuhamia Jimbo la Zamfara ambapo alifanikiwa kupata nafasi ya kujiunga na Savannah Scorpions ya Gombe United, ambapo aliwasaidia kupanda daraja kuingia katika ligi ya NPFL mwaka 2020. Akiwa anacheza Gombe United, Abdulazeez alimaliza kama mfungaji wa pili bora zaidi katika Ligi ya Soka ya Kulipwa ya Nigeria ya mwaka 2021-2022, akifunga magoli 16, magoli matatu nyuma ya mfungaji bora wa ligi, Chijioke Akuneto wa Rivers United.

Usajili kwenda klabu ya Kishwidi ya Mjällby AIF ya ligi ya Allsvenskan ulikubaliwa mwezi Septemba 2022. Alikamilisha mkataba wa miaka mitatu ambao utamweka Listerlandet hadi mwaka 2025. Safari yake ya soka ilianzia katika ligi ya Mjälby tarehe 16 Oktoba 2022 katika kipigo cha nyumbani cha 3-0 dhidi ya Hammarby Fotboll.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yusuf Abdulazeez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.