Zaire
Zaire ni neno lenye maana mbalimbali:
- kiasili ni jina la kihistoria kwa ajili ya mto Kongo. Wareno walitamka neno la Kibantu la "nzari" (=mto) kama "zari - zaire".
- watu wa nje wakati mwingine walitumia jina la mto pia kwa ajili ya ufalme wa Kongo ulioenea pande zote mbili za mto.
- jina la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati 27 Oktoba 1971 na 17 Mei 1997
- Zaire ilikuwa pesa ya Kongo wakati ilipoitwa "Zaire"
- jina la mkoa mmoja wa Angola
- jina la mkoa wa Bas-Zaire katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hadi mwaka 2007.
Viungo vya Nje