Ziwa Poyang
Ziwa Poyang ndilo ziwa kubwa zaidi la maji safi nchini China. Linapatikana katika Jimbo la Jiangxi. Ziwa hilo linapokea maji yake hasa kutoka mto Gan, pamoja na mito ya Xin na Xiu. Gan inatoka tena ziwani na kupeleka maji yake kwenda mto Yangtze.
| |
Eneo la maji | km2 3,210 |
Kina cha chini | m 8-25 |
Mito inayoingia | Mto Gan |
Mito inayotoka | Mto Gan |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
m 16.5 |
Kiasi cha maji kwenye ziwa hilo hubadilikabadilika kufuatana na majira na hivyo ukubwa wake huchezacheza. Kwa sasa ukubwa wa kawaida ni mnamo km2 3210 lakini mwaka 2016 lilipungua hadi kuwa na km2 200 pekee. Lilipungua tangu kuundwa kwa Lambo la Magenge Matatu kwenye mto Yangtse.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Poyang kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |