Zuchu

Mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo wa Tanzania
(Elekezwa kutoka Zuhura Kopa)

'

Zuhura Othman Soud
Amezaliwa12 Oktoba 1993 (1993-22-12) (umri 30)
Majina mengineZuchu
Kazi yakeMsanii


Zuhura Othman Soud (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Zuchu; alizaliwa 22 Novemba 1993[1]) ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo na msanii wa kurekodi wa Kitanzania aliezaliwa Zanzibar. Amesainiwa chini ya lebo ya WCB Wasafi Records chini ya uongozi wa Diamond Platnumz. [2] [3][4]

Alitunukiwa tuzo ya silver play button na mtandao wa kijamii wa Youtube kwa kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika mashariki kwa kufikisha wafuasi zaidi ya 100,000 ndani ya wiki moja.[5]

Katika wiki ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa, Zuchu alitunukiwa tuzo ya msanii bora chipukizi wa mwaka 2020 na All Africa Music Awards|AFRIMMA.[6]

Maisha ya awali hariri

Zuchu amezaliwa kwenye familia ya wanamuziki . Ni binti wa mwanamuziki wa taarabu anayefahamika kwa jina la Khadija Kopa.[7][8][9][10] Zuchu alianza kuimba akiwa na umri mdogo na baadae kushirikiana na mama yake Khadija Kopa katika wimbo unaofahamika kama Mauzauza [11]

Zuchu alitambulika rasmi kwenye Tasnia ya muziki mnamo Aprili 2020. [12] Mpaka sasa ana albamu moja na alichaguliwa kushiriki mashindano ya kuwania tuzo ya MTV, MAMA awards ya mwaka 2021. Kwenye mashindano hayo, Zuchu amepangwa katika kipengele cha 'best breakthrough act', anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Elaine na Focalistic wa Afrika Kusini na Tems na Omah Lay wote kutoka Nigeria, John Blaq (Uganda) na Sha Sha (Zimbabwe). Mpaka sasa ana albamu moja na alichaguliwa kushiriki mashindano ya kuwania tuzo ya MTV, MAMA awards ya mwaka 2021. Kwenye mashindano hayo, Zuchu amepangwa katika kipengele cha 'best breakthrough act', anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Elaine na Focalistic wa Afrika Kusini na Tems na Omah Lay wote kutoka Nigeria, John Blaq (Uganda) na Sha Sha (Zimbabwe).[13]

Albamu hariri

Zuchu aliachia albamu ya kwanza iliyotambulika kama “ I am Zuchu “ mwaka 2020 ikiwa na nyimbo 7. [14] Albamu yake ndiyo iliyosikilizwa na watu wengi zaidi nchini Tanzania kwa mwaka 2020 na vidio za nyimbo zake zimetazamwa na mamilioni ya watu.[15]

Nyimbo zake hariri

Mwaka Nyimbo Albamu
2020
"Hakuna Kulala" I Am Zuchu EP
"Nisamehe"
"Kwaru"
"Wana"
"Raha"
"Ashua"(feat. Mbosso)
"Tanzania ya Sasa"
"Shangilia"
"Mauzauza"(feat. Khadija Kopa)
"Cheche" (feat. Diamond Platnumz)
"Litawachoma" (feat. Diamond Platnumz)
"Hasara"
"Nobody" (feat. Joeboy)
2021
"Sukari"

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zuchu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.