Edward Cummings

(Elekezwa kutoka E. e. cummings)

Edward Estlin Cummings (kwa kifupi E. E. Cummings; 14 Oktoba 1894 - 3 Septemba 1962) alikuwa mshairi na mwandishi mashuhuri kutoka Marekani. Kwa jumla aliandika na kuchapisha mashairi, riwaya na tamthilia mia tisa. Vile vile, Cummings alijulikana sana kama mchoraji wa picha kadhaa zilizovutia.

Edward Cummings.

Mashairi ya Cummings yaligusia sana masuala ya mapenzi na mazingira - alipenda sana kuandika juu ya majira ya kuchipua. Mashairi yake yalipata umaarufu kwa sababu hayakuakifishwa kama ilivyo kawaida.

Watalaamu wengi wanaamini kuwa Cummings alikuwa mmojawapo wa washairi waliojulikana sana kule Marekani katika karne ya 20. Mashairi aliyoandika Cummings, na ambayo yanajulikana sana, ni kama: "In Just Spring", "A Man Who Had Fallen Amongst Thieves", "The Cambridge Ladies" na "Buffalo Bill".

Vitabu

hariri


Baadhi ya tuzo alizopewa

hariri

Marejeo

hariri
  1. "E. E. Cummings". Poetry Foundation. Poetry Foundation. Aprili 19, 2018. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: others (link)
  2. 2.0 2.1 "John Simon Guggenheim Foundation | E. E. Cummings".
  3. "Shelley Winners – Poetry Society of America". poetrysociety.org. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2018. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |website= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "POETRY AWARD IS MADE; E.E. Cummings Wins the 1950 Harriet Monroe Prize", The New York Times, June 11, 1950. 
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 Cummings, E. E. (Februari 4, 2014). "E. E. Cummings". E. E. Cummings. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edward Cummings kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.