"Ghetto Gospel" ni wimbo wa rapa Tupac Shakur, ambo ulitolewa kama single ya pili baada ya kufa kwake. Wimbo unatoka katika albamu mwaka wa 2004, Loyal to the Game. Wimbo ulitungwa na Tupac Shakur ukiwa kama kilio cha "kumaliza vita mitaani", unalenga hasa utofauti wa ubaguzi wa rangu usio na maana na upingaji wa sera za haki za binadamu, hasa kwa wale walio-maskini mno. Wimbo umeshirikisha kibao cha Elton John cha Indian Sunset. Kwenye Ghetto Gospel 2pac anaelezea kinagaubaga kuhusu maisha ya watu wanaoishi ghetto. Wimbo umetayarishwa na Eminem. "Ghetto Gospel" ulikuwa wimbo pekee kutoka kwenye Loyal to the Game ukisindikizwa na muziki wa video. Mwishoni kabisa mwa video kuna ujumbe kutoka kwa mama'ke, Afeni Shakur, akisema "Kumbuka kujiweka hai, kwani hakuna muhimu zaidi ya hicho." Wimbo ulifikia nafasi ya #1 kwenye chati za UK, baada ya chini zaidi ya mwaka, rapa mhasimu The Notorious B.I.G. amefikia nafasi #1 na single yake ya Nasty Girl.

“Ghetto Gospel”
“Ghetto Gospel” cover
Single ya 2Pac akishirikiana na Elton John
kutoka katika albamu ya Loyal To The Game na Best of 2Pac Part 2 - Life
B-side "Thugs Get Lonely Too"
Imetolewa 21 Agosti 2005
Muundo CD
Aina West Coast hip hop, conscious hip hop
Urefu 3:58
Mtunzi Tupac Shakur, Elton John, Bernie Taupin
Mtayarishaji Eminem
2Pac single 2Pac akishirikiana na Elton John
"Thugs Get Lonely Too"
(2004)
"Ghetto Gospel"
(2005)
"Untouchable"
(2006)
Mwenendo wa single za Elton John
"Turn the Lights Off When You Leave"
(2005)
"Ghetto Gospel"
(2005)
"Electricity"
(2005)

Orodha ya nyimbo hariri

CD single
# JinaMtunzi (wa)Sampuli Urefu
1. "Ghetto Gospel" (akim. Elton John)  3:58
UK CD single
# JinaMtunzi (wa)Mtayarishaji Urefu
1. "Ghetto Gospel" (akim. Elton John) Eminem 3:58
2. "Thugs Get Lonely Too" (akim. Nate Dogg) Eminem 4:48

Pia kulikuwa na toleo ambalo hakumshirikisha Elton John.

Michakaliko ya Chati hariri

Ilifika nafasi ya #3 kwenye chati European Hot 100 Singles ambapo ilikaa kwa majuma mawili.

Chati Nafasi
Australian Singles Chart
1
Austrian Singles Chart
3
Belgian Singles Chart
25
Danish Singles Chart
20
Irish Singles Chart
1
New Zealand Singles Chart
3
Swiss Singles Chart
7
UK Singles Chart
1
Billboard European Hot 100
3

Tanbihi hariri

Marejeo hariri