Kalemie

mji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo


Kalemie ni mji wa J.K. Kongo uliopo kando ya ziwa Tanganyika upande wa magharibi kwa kimo cha mita 785 juu ya UB pale ambako mto Lukuga unapotoka ziwani. Mwaka 2005 Kalemie ilikuwa na wakazi 147,000. Kuna bandari muhimu yenye mawasiliano kwa meli na Kigoma (Tanzania) na Bujumbura (Burundi).

Kalemie
Kalemie is located in Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kalemie
Kalemie

Mahali pa mji wa Kalemie katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Majiranukta: 05°56′0″S 29°12′0″E / 5.93333°S 29.20000°E / -5.93333; 29.20000
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mkoa Mkoa wa Tanganyika
Idadi ya wakazi (2012)
 - Wakazi kwa ujumla 146,974
Sokoni ya Maendeleo

Kalemie iliundwa kama kituo cha kijeshi tarehe 30 Desemba 1891 upande wa kusini wa chanzo cha mto Lukuga ziwani na kapteni Mbelgiji Jacques de Dixmude kwa jina la Albertville kwa heshima ya mfalme mtarajiwa Albert wa Ubelgiji. Mji ulikua baada ya kufika kwa reli ya Kongo.

Kalemie ni mwisho wa reli; mipango ya kale ya ukoloni ilikuwa kwamba njia ya reli kutoka Atlantiki ingeishia hapa itakayoounganishwa kwa feri na bandari ya Kigoma penye chanzo cha reli ya Tanganyika kwenda Dar es Salaam. Kutokana na miaka mingi ya fujo reli ya Kongo haikukamilishwa kamwe: haifiki hadi Atlantiki lakini kuna njia ya reli kuanzia Kalemie hadi jimbo la Katanga.

Kuna viwanda vya nguo na saruji.

Mwaka 2005 mji uliathiriwa na tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kalemie kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.