Lango:Afrika/Makala iliyochaguliwa

Makala iliyochaguliwa hariri

Makala iliyochaguliwa kwa Mei 2012 hariri

 
Eneo la Zanj ya kihistoria kwenye ramani ya Afrika ya Mashariki

Zanj (Kiarabu na Kifarsi زنج) ni neno lililotumiwa na waandishi Waislamu wa zamani kutaja watu weusi kutoka Afrika ya Mashariki na pia kwa maana ya kijiografia kutaja eneo la Afrika ya Mashariki. Wanajiografia Waislamu walihesabu pwani takriban kati ya Mogadishu na kisiwa cha Pemba kuwa "Zanj". Kusini yake waliita nchji ya Sofala na kaskazini yake nchi ya Berbera kufuatana na mabandari ya nyakati ziule zilizojulikana kwao. Uwezekano mkubwa ni neno hili Zanj latokana na jina la kijiografia la awali "Azania" likatumiwa baadaye kutaja hasa kisiwa cha Zanzibar. Baadaye Zanj imejulikana kama nchi ya Waswahili. Waandishi Waarabu wa kale waliita hasa watu weusi kutoka Afrika ya Mashariki kwa jina hili la "Zanj". Waliwatofautiana na Waafrika weusi wengine kama Wanubia (taz. Nubia) au Wahabash (taz. Uhabeshi). Walitazamiwa kuwa watu wenye hali na maendeleo ya duni kulingana na wenyeji wengine wa Afrika iliyojulikana kwa Waarabu.