Masista Waminimi wa Bikira Maria wa Mateso

Masista Waminimi wa Bikira Maria wa Mateso wanaunda shirika la kitawa lenye hadhi ya Kipapa.[1]

Historia hariri

 
Mt. Klelia Barbieri, mwanzilishi.

Tarehe 1 Mei 1868 Klelia Barbieri (1847-1870) na wenzake watatu, chini ya paroko Gaetano Guidi, walianza kuishi kijumuia katika nyumba karibu na kanisa la Le Budrie, kitongoji cha San Giovanni in Persiceto (Bologna, Italia).

Walikuwa wanafundisha katekisimu na kuandaa watoto kupokea sakramenti.

Jumuia iliitwa ya Waminimi kwa heshima ya Fransisko wa Paola na ya Bikira Maria wa Mateso kutokana na Bikira Maria aliyeheshimiwa hivyo katika parokia hiyo.[2]

Kardinali Lucido Maria Parocchi alikubali kwa jaribio shirika hilo jipya tarehe 26 Oktoba 1879, halafu mwandamizi wake katika Jimbo kuu la Bologna, kardinali Domenico Svampa, alilipatia hadhi ya kijimbo.[2]

Shirika lilihusianishwa na utawa wa Watumishi wa Maria tarehe 9 Januari 1951, likapata decretum laudis tarehe 20 Machi 1934 likakubaliwa moja kwa moja kuwa la Kipapa tarehe 24 Januari 1949.[2]

Klelia Barbieri alitangazwa mwenye heri mwaka 1968, na mtakatifu mwaka 1989.

Uenezi hariri

Mbali ya Italia, ambako yako makao makuu huko Bologna, masista siku hizi wako pia Brazil, India na Tanzania.[1]

Mwishoni mwa mwaka 2008 walikuwa 294 katika jumuia 36.[1]

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 Ann. Pont. 2010, p. 1497.
  2. 2.0 2.1 2.2 A.M. Galuzzi, DIP, vol. V (1978), coll. 1348-1349.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri