Mtumiaji:Muddyb/Mali Zangu Zimeniangamiza

Mali Zangu Zimeniangamiza
Jalada la Mali Zangu Zimeniangamiza
MwandishiMuddyb Mwanaharakati
Msanii wa kavaKindo Emmanuel
NchiTanzania
LughaKiswahili
AinaKusisimua
Set inKimanzichana
Kimechapishwa2019
MchapishajiDar General Publishing House
Tarehe ya kuchapishwa
8 Januari, 2019
Aina ya MediaKaratasi
Kurasa110
ISBN978-9976-5467-0-5

"Mali Zangu Zimeniangamiza" ni jina la kitabu cha riwaya kutoka kwa mchangiaji wa kujitolea wa Wikipedia ya Kiswahili, mchambuzi wa masuala ya muziki na filamu na masuala mengine ya kijami. Hii ni riwaya ya kwanza kutoka kwa Muddyb. Riwaya imetoka tarehe 8 Januari, 2019. Mwandishi anamwelezea kijana Hamisi Manga mwenye makazi yake huko Kimanzichana, Mkuranga Pwani, Tanzania. Kijana huyu aliyekuwa anafanya kazi kuuza vinywaji baridi na baadaye kuongeza juhudi katika kazi na hatimaye kuwa na pesa nyingi sana kwa kuanza kidogo-kidogo.

Muhtasari wa hadithi hariri

Hamisi na Mwanaidi Manga ni watoto wa mzee Hassan Mbutike Manga wa Kimanzichana, Mkuranga Pwani. Wanazaliwa na mama mmoja, lakini hakudumu katika ndoa kisha mama yao anaenda kuolewa na mwanaume mwengine kwa sababu ya kipato cha mzee Manga kuanza kuwa hafifu. Hamisi ni mfanyabiashara ndogo-ndogo maarufu mmachinga, hukohuko kwao Kimanzichana. Ni kijana mtiifu na mwerevu wa mambo mengi mno. Ana akili na uthubutu wa hali ya juu katika mambo mengi sana. Siku moja anaamka anasogea kijiweni kwake, hakuti vijana wenzake wanaojishughulisha na kazi za uuzaji vinywaji. Anatafakari na kuchungua kipi kilichopelekea kutokuwepo kwa vijana wenzake pale kijiweni, hatimaye anaupata ukweli ni kwamba walikimbiza mwizi na kumpeleka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa. Katika sakata hilo lililohusisha mtoto wa mwenyekiti na kesi ya kwiba. Huko yaliyowakuta ni makubwa na kutakiwa kutojishughulisha na chochote katika eneo la barabara kuu ya kwenda Dar es Salaam na Kisiju Pwani. Tukio hili la aina yake, linakuwa baya kwa vijana wenzake, lakini ni mtaji mkubwa kwake, kwani ilipelekea kuwa muuzaji pekee katika kituo cha mabasi na hatimaye kuhudumia watu wote barabarabani. Juhudi na uaminifu unapelekea kuanzisha urafiki wa karibu na mwuzaji maarufu wa jumla na rejereja Mwarabu.

Ukaribu na heshima ya Hamisi unapekea kupata mafanikio makubwa kabisa. Akaja kuwa mwuzaji mkubwa sana Chamanzi, baadaye kupanua wigo wa biashara zake huko Kisiju Pwani na Dar. Umri unasogea anaoa, anapata mtoto, halafu balaa linaanzia hapa. Kwa utajiri alionao, alipata misukosuko mingi sana, Alipambana kwa namna alivyoweza, lakini hakuweza kushindana na hasadi hizo mwishowe kaondoka duniani.

Waliofanikisha mauti yake, hawakufaidi chochote kile licha ya kuwa na matumaini ya kupata mgao mkubwa. Mambo yote aliacha kisheria na hakuna wa kuyapangua.

Wahusika hariri

  • Hamisi Manga: Machinga aliyekuja kuwa tajiri mkubwa Kimanzichana na Kisiju. Katika riwaya Hamisi anaonekana kuwa mfanyaji kazi mwenye juhudi ya juu sana na mwenye nafsi fulani ya upendo kwa ndugu, jamaa, marafiki na watu wengine mbali na wale anaofahamiana nao. Vilevile uaminifu katika kazi unamfanya kuwa kipenzi kikubwa cha Mwarabu.
  • Mwarabu: Tajiri wa kijijini ambaye alijenga ukaribu sana na Hamisi hadi kupelekea kumpa bidhaa zake kwa mali kauli. Mwarabu ndiye hasa kiini cha utajiri wa Hamisi. Alimpenda Hamisi na kumpa kila alichotaka kwa makubaliano ya kununua kila kitu katika maduka yake.
  • Rama: Huyu ni kijana yatima anayeishi na mjombake huko Kimanzichana. Hamisi anamchukua Rama kama msaidizi wake baada ya biashara kuanza kukua na kumuelemea. Rama ni kama toleo la pili la Hamisi. Mchapakazi, ana roho nzuri na anapendwa sana na wazee kwa vijana pale Kimanzichana. Baadaye sana anakuja kumuoa Mwanaidi kwa ushauri wa Hamisi ili wazitunze mali zao za Kisiju Pwani.
  • Mwanaidi: Mdogo wake Hamisi. Anazaliwa tumbo moja na Hamisi. Mpole na mtiifu. Awali alikuwa anashinda nyumbani tu hadi hapo Hamisi alipomkabidhi ukubwa na usimamizi wa mali zake za Kisiju Pwani. Baadaye anakuja kuoelewa na Rama kwa ushauri wa Hamisi ili kuondoa mkanganyiko wa mali zake.
  • Mzee Manga: Baba yake Hamisi na Mwanaidi Manga. Baba mwenye busara na hikima. Ameonesha misimamo yake ya waziwazi dhidi ya mke wake wa zamani­­­-mama Hamisi. Alimsihi sana mwanawe awe mbali na mama yake, lakini sikio la kufa halisikii dawa.
  • Mama Hamisi: Mama mzindaki, mpenda pesa, asiyependa maendeleo ya watoto zake wa mume wa kwanza Mzee Manga. Mama baadaye atajaribu kufitinisha ndoa ya Hamisi, lakini mambo yatamwendea kombo na hatimaye kufurumushwa na Hamisi asikanyage kwake wala wasijuane. Anaishia kupata fadhaa ya maisha kwa roho mbaya aliyonayo.
  • Zawadi Dieni: Mke wa Hamisi na mama yake mzazi Tarqui Hamisi. Mwanamke aliyebeba nembo ya uimara na msimamo katika ndoa. Hakubali kuyumbishwa hata kidogo.
  • Mzee Kimosa: Mlinzi na baba mlezi wa Hamisi katika mji wake. Kazi kubwa ya Kimosa ni kulinda tu, lakini vilevile Hamisi alimtaka ahusike moja kwa moja na maisha yake binafsi mbali na ulinzi.
  • Hamida: Mfanyakazi wa ndani wa Hamisi. Hamisi anamwita dada HAMIDA kwa sababu kamzidi kiumri na amefika zaidi ya miaka arobaini na kitu. Alimleta kama msaidizi kwa mkewe na humfanya kama dada yao na si mfanyakazi wao.
  • Mwinshehe: Mdogo wake Hamisi wa mama mmoja-baba tofauti.
  • Mzee Hamisi: Mzee aliyewakaribisha na kuwaonesha mji akina Hamisi na Rama huko Kisiju Pwani.

Marejeo hariri