Nyanda za juu za Ngorongoro
Nyanda za juu za Ngorongoro (kwa Kiingereza: Ngorongoro Highlands au Crater Highlands) ni eneo lenye miinuko lililopo kwenye bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki katika mikoa ya Arusha na Manyara, kaskazini mwa Tanzania.
Jiolojia hariri
Nyanda za juu za Ngorongoro zinapatikana katika mgawanyiko ambapo bamba la Afrika linagusana na bamba la Somalia, kukutana kwa mabamba haya mawili husababisha maumbile mapya ya kijiolojia kujitokeza.[1]
Kama ilivyo kawaida, sehemu za mgawanyiko kati ya mabamba ya gandunia, maumbile ya kivolkeno huwepo. Hivyo nyanda hizo zina kasoko nyingi na kaldera za kivolkeno. Magma, hupanda kupitia nyufa zilizotokea na kufika kwenye uso wa ardhi na kuunda umbo la koni. Kaldera huundwa pindi volkeno ikilipuka au kuporomoka ndani yake.[1]
Jiografia hariri
Yafuatayo hupatikana kwenye nyanda za juu za Ngorongoro:
Tazama pia hariri
Marejeo hariri
- ↑ 1.0 1.1 "Crater Highlands". NASA Earth Observatory. Iliwekwa mnamo 29 September 2017. Check date values in:
|accessdate=
(help)
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |