Reggie Tsiboe (alizaliwa 7 Septemba, 1964), ni Mghana-Mwingereza mburudishaji , dansi na mmoja wa waimbaji wa kikundi cha disko Boney M. kati ya mwaka 1982 na 1986 na baadaye kati ya mwaka 1989 na mwaka 1990[1][2].

Mwaka 1982, Tsiboe alichukua nafasi ya mchezaji densi Bobby Farrell, lakini mnamo 1984 Farrell alijiunga tena na kikundi na wakawa wanadensi kwa pamoja[3]. Mwaka 1986, bendi ya asili iligawanyika baada ya miaka 10 ya mafanikio, lakini mwaka wa 1989, Liz Mitchell na Reggie waliunda toleo jipya rasmi la Boney M. na mwaka wa 1990 walitoa nyimbo kwa msaada wa mtayarishaji Frank Farian "Hadithi", lakini miezi michache baadaye wote wawili walienda njia zao tofauti.

Tsiboe alionekana kwenye albamu tatu za mwisho za Boney M.: Ten Thousand Lightyears (1984), Kalimba de Luna - 16 Happy Songs (1984) na Eye Dance (1985) na pia alirekodi nyimbo za Krismasi na kikundi, ambazo zilitolewa kimataifa baada ya mgawanyiko wa bendi kwenye albamu mpya ya Boney M. Christmas, Nyimbo 20 kubwa za krismasi mwaka wa 1986. Reggie aliimba sauti kuu za nyimbo kadhaa za Boney M, zikiwemo "Kalimba de Luna", "Happy Song", "Going Back West", "My Chérie Amour", "Young, Free and single", "Dreadlock Holiday" na "Barbarella Fortuneteller.

Tarehe 21 Septemba 2006, Tsiboe na waimbaji wengine wawili wakuu wa Boney M., Liz Mitchell na Marcia Barrett, walikuwa wageni maalum huko London kwenye onyesho la kwanza la muziki la Daddy Cool, ambalo lilitokana na muziki wa kikundi hicho maarufu.

Kabla ya kujiunga na kundi hilo alikuwa mwigizaji wa filamu nchini Ghana. Moja ya filamu iliyompa umaarufu ni filamu ya Love Brewed in an African Pot. Kufuatia kipindi chake cha Boney M Tsiboe alirejea katika uigizaji, Pia ameigiza katika filamu chache za TV za Uingereza Akiwemo Dr who.

Tsiboe sasa anaishi Marlborough, Wiltshire nchini Uingereza.

Marejeo hariri

  1. "Reggie Tsiboe, Biography". www.ghanaweb.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-26. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  2. https://boneym.es/bio-reggie-tsiboe/
  3. https://books.google.com/books?id=IwkKAQAAMAAJ&q=Reggie+Tsiboe