AFC Leopards SC , mara nyingi hujulikana kama "AFC" au "the Leopards," ni klabu ya soka, mjini Nairobi, ambayo ilianzishwa mwaka wa 1964. Jina lake lingine ni "ingwe" ( "chui" katika lugha ya Kiluhya), ni klabu maarufu na ya kitamaduni ya Kenya na uwanja wake wa nyumbani ni Uwanja wa Taifa wa Nyayo, ambayo ina nafasi ya watu 30000. Licha ya kuwa na makao katika mji mkuu, Nairobi katika sehemu ya kusini mashariki, ushabiki wake kwa wingi hutoka mkoa wa magharibi. Timu huvalia jesi nyeupe , vinyasa vyeupe na soksi za bluu na wakati mwingine na shati yenye rangi ya bluu na nyeupe; nguo mbadala ni jesi nyekundu na vinyasa vyeupe. Mpinzani wake wa jadi ni Gör Mahia; makabiliano yao hufurahisha sana, na kutokana na mapenzi ya mashabiki makabiliano ya hawa wawili huchukuliwa kama "derby" maarufu na makali zaidi katika kanda. AFC inachukuliwa kama timu hatari ya Afrika ya mashariki, ya kati na ya kusini kwa sababu ya mechi nyingi ambazo imecheza barani na utawala wake katika michuano ya klabu ya CECAFA, kwa kuongezea wachezaji wake wazuri.

AFC Leopards
Rangi nyumbani
Rangi za safari

Historia

hariri

AFC Leopards ni mmojwapo wa vilabu ambavyo vimefanikio zaidi katika kanda na hii ni ukweli kutokana mataji 12 ya ligi ambayo klabu hii imeshinda na kombe la Kenya mara 6 pamoja na shindano la klabu la CECAFA mara 5. Klabu hii ilianzishwa mwaka wa 1964 kama Abaluhya United FC wakati idadi ndogo ya vilabu viliungana Jina lilibadilishwa kuwa Abaluhya FC na baadaye kuwa All Footballers Federation-AFC, bado inadumisha AFC (na ikawa AFC leopards) mwaka wa 1980, wakati serikali ya Kenya ilipiga marufuku majina ya kikabila (Abaluhya inaashiria kabila ya Waluhya). Kama klabu nyingi za Kitamaduni za Kenya, AFC Leopards ilikabiliwa na matatizo ya kifedha kutokana na usimamizi mbaya.Udanganyifuu uliyozunguka mwenendo wa Ligi Kuu ilikamillika na klabu ilienda katika ligi ya chini Kwa sababu ya suala hili klabu hii haikushiriki katika ligi yoyote katika mwaka 2007 lakini ilishiriki sehemu katika kombe la KFF Community ambayo ilianzisha makali yake. Mwaka wa 2008 timu hii ilishiriki katika ligi ya Nationwide, ligi ya pili nchini Kenya na ilishinda katika eneo lao, na hivyo basi kurejea katika Ligi kuu ya Kenya kwa msimu wa 2009 Hata hivyo,"ingwe" imeimarishwe kiwango kinachoheshimika cha kucheza na bado kinashikilia tamaduni ya kihistoria kama timu.

Mwaka wa 2009 timu ilishinda Kombe la Kenya baada ya miaka nane kavu bila kombe lolote. Hata hivyo, vilabu vingine viligoma kushiriki katika kombe hilo

Ufuasi

hariri

AFC Leopards SC ina wafuasi wengi tofauti, ambao wanaupinzani mkubwa na vilbu vingine, hasa Gör Mahia. Inaweza kupingwa kuwa klabu hii ndiyo kubwa zaidi na maarufu nchini Kenya na Afrika ya Mashariki – lina wafuasi waliokadiriwa kuwa milioni 6 nchini Kenya. Mashabiki hawa wanajumuishwa katika matawi ya wafuasi yaliyoenea kote nchini. Hata hivyo, ufuasi na umaarufu wake unapita mipaka ya Kenya hadi wa bara zima sansana Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika. Kiakili, klabu maarufu zaidi Kenya na Afrika ya Mashariki kamwe halijwahi kucheza mechi ya ugenini - AFC Leopards SC hupata wafuasi zaidi katika mechi za ugenini kuliko timu za upinzani za nyumbani..Hata kwa sasa bado klabu hii inadumisha wastani wa juu zaidi wa kutazamwa na wafuasi wao kuliko vilabu vingine vyote vya Ligi Kuu ya Kenya.Mechi yao ya kwanza waliporudi katika Ligi Kuu mwaka wa 2009 ilibidi isimamishwe kwa sababu ya uhaba wa usalama ulyosababishwa kwa kuanguka kwa mzunguko kutokana na umati wa wafuasi wake ndani na nje ya uwanja.

Majilio

hariri
  • Ligi kuu ya Kenya
1966, 1967, 1970, 1973, 1980, 1981, 1982, 1986, 1988, 1989, 1992, 1998
  • Kombe la Rais
1967, 1968, 1985, 1991, 1994, 2001, 2009
  • Kombe la klabu la CECAFA
1979, 1982, 1983, 1984, 1997

Utendaji katika mashindano ya CAF

hariri
  • Ligi ya Mabingwa ya CAF
1999 - Raundi ya Kwanza
  • Kombe la Mabingwa wa klabu la Afrika : Matokeo 12

1968: Nusu fainali
1971: Raundi ya kwanza
1972: Ilijitoa katika raundi ya kwanza
1974: Robo fainali

1981: Raundi ya kwanza
1982: Raundi ya kwanza
1983: Raundi ya kwanza
1984: Raundi ya kwanza

1987: Raundi ya pili
1989: Raundi ya pili
1990: Robo fainali
1993: Raundi ya kwanza

  • Kombe la CAF : Matokeo 2
1994 - robo fainali
1997 - robo fainali
  • Kombe la CAF la washindi:Matokeo 5

1985 - Nusu fainali
1986 - Raundi ya Pili

1988 - robo fainali
1992 - Raundi ya Kwanza

2002 - Raundi ya kwanza

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri