Gör Mahia
Gör Mahia ni klabu ya kandanda yenye makao yake katika mji mkuu wa Nairobi nchini Kenya. Ni kimojawapo kati ya vilabu viwili maarufu zaidi nchini katika kandanda ya vilabu nchini Kenya (klabu nyingine maarufu na mpinzani wake wa jadi ni AFC Leopards).
|
Gör Mahia imeshinda Ligi ya Kenya mara 21 na Kombe la Kenya mara nane. Gör Mahia ndiyo klabu ya kipekee nchini Kenya kushinda Taji la bara Afrika, kwani klabu hii ilishinda Kombe la Afrika la mabingwa mwaka wa 1987. Klabu hii ilianzishwa mwaka wa 1968 wakati vilabu viwili vya kandanda,Luo United na Luo Sports Club (pia ilikuwa inajulikana kama Luo Stars) , viliungana. Mmoja wa mwanzilishi wake alikuwa mwanasiasa Tom Mboya. Uwanja wao wa kucheza mechi za nyumbani ni Nairobi City Stadium.
Gör Mahia imeshinda shindano moja tu tangu mwaka wa 1995. Aidha, imeepuka kuteremshwa kwa ligi ya divisheni ya pili mara tatu. Licha ya matatizo yake ya kifedha, klabu hii ilikuwa inacheza vyema katika ligi msimu wa 2005-2006 lakini hatimaye mabishano mapya yaliharibu kila kitu.
Gör Mahia kama klabu inamizizi ya hekaya, hadithi na simulizi za Kiluo. Gör Mahia alikuwa shujaa wa Kiluo ambaye alikuwa anajulikana kwa umiliki wake wa mamlaka ambayo yalimwezesha kufanya maajabu. Mahia ni neno la Kiluo ambalo linaelezea ajabu na siri na hivyo basi wakati Gör ilianzishwa ilitakiwa kumiliki sifa asili za Gor Mahia kutokana na jina lake. Hakika Gör iliweza kudhibiti jina hilo na hata kupitisha matumaini ambayo watu wengi walitarajia. Katika miaka yake ya mafanikio, hakuna timu iliyoweza kupambana za Gör na baadhi ya watu waliona klabu hii kuwa bora barani Afrika. Sambamba na uaminifu wa wafuasi wake, Gör bado ina uwezo wa kusimama kutoka kwenye majivu na kurejea utukufuni walioupoteza kama "Gör wenye nguvu".
Klabu hii ilirejesha sifa yake ya kupata mataji mwaka wa 2008 wakati ilishinda Kombe la KFF. Hata hivyo, klabu zingine zote za KPL ziligoma kushiriki katika kombe hilo.
Majalio
hariri- African Cup Winners 'Cup
- 1 (1987)
- Kombe la klabu za CECAFA
- 3 (1980,1981,1985)
- Ligi kuu ya Kenya
- 21 (1968, 1974, 1976, 1979, 1983, 1984, 1985, 1987, 1990, 1991, 1993, 1995, 2013, 2014, 2015, 2017, 2018, 2019, 2020, 2023, 2024)
- Kombe la KFF Cup
- 8 (1976, 1981, 1983, 1986, 1987, 1988, 1992, 2008)
- Kenya Super Cup
- 1 (2009)[1]
Utendaji katika mashindano ya CAF.
hariri- Kombe la shirikisho la CAF : tokeo 1
-
- 2008 - Raundi ya mchujo
- Kombe la Mabingwa wa klabu la Afrika : Matokeo 8
|
|
|
- Kombe la CAF : Matokeo 2
- 1974: Robo fainali
- 1971: Raundi ya kwanza
- Kombe la CAF la washindi:7
|
|
|
Marejeo
hariri- ↑ tovuti ya Daily Nation tovuti, 24 Januari 2009 Gor tear Mathare United apart