Mkutano wa mawaziri wa Afrika kuhusu mazingira
(Elekezwa kutoka AMCEN)
Mkutano wa mawaziri wa Afrika kuhusu mazingira (African Ministerial Conference on the Environment kifupi AMCEN) ni ushirikiano wa mawaziri husika wa nchi za Afrika.
Mawaziri hao walikutana mara ya kwanza mwaka 1985 mjini Kairo, Misri. Baadaye mkutano ulianzishwa kama taasisi ya kudumu mwenye shabaha ya
- Kuunganisha jitihada za hifadhi ya mazingira
- kuunganisha kinga ya mazingira na kupatikana kwa mahitaji ya kimsingi ya wananchi kwa namna ya uendelevu
- kuhakikisha kuwa kilimo kinalingana na mahitaji ya uhakika wa chakula wa Afrika
AMCEN ilishiriki katika maandalizi ya mradi wa New Partnership for Africa 's Development (NEPAD) upande wa mazingira.
Mkutano unashirikiana na Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (UNEP).
Masahihisho ya Mkataba wa Afrika kuhusu hifadhi ya mazingira na maliasili yaliandaliwa katika AMCEN.
Mkutano wa mawaziri unafanyika kila baada ya miaka miwili. Ofisi ya UNEP-Afrika inatoa huduma ya ofisi ya kudumu kwa AMCEN pia.