Absalomu Nyinza, maarufu Abbi, ni mwanamuziki wa mtindo wa Afro-jazz na Afro-fusion kutoka Kenya. Yeye huambatana na bendi ya Kikwetu . Huimba katika lugha kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, lugha yake ya mama Kiluhya na lugha za makabila mengine.

Abbi ilianza kazi yake mwaka wa 1993 akiwa mwanachama wa kundi la injili la a cappella la The Boyz ambalo baadaye lilibadili jina hadi Safari . Alizuru Uingereza na Ujerumani akiwa na hiyo bendi. Baadaye alijunga na bendi ya Achieng Abura , na kuzuru Uhispania wakati huo .[1]

Solo albamu yake, Mudunia ilitolewa mwaka 2003. Katika Tuzo za Muziki za Kisima za 2004, alishinda katika vitengo viwili: Msanii Bora wa Kiume na Msanii bora anayechipuka . Albamu yake ya pili Indigo ilitolewa mwezi Agosti 2007. Ametumbuiza katika tamasha za Festival Mundial na North Sea Jazz nchini Uholanzi na kuzuru nchi nyingine pia.[2] Muziki wake hutayarishwa na Tedd Josiah wa Blu Zebra studio [3].

Amekampeinia kundi la Global Call to Action Against Poverty [4]. Yeye ni miongoni mwa wasanii wa Kenya ambao wamefadhiliwa na Alliance Française mjini Nairobi [5].

Marejeo hariri

  1. Italian Cultural Institute in Nairobi Abbi & Kikwetu in concert Archived 22 Julai 2011 at the Wayback Machine.
  2. Word Music Central - Abbi. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-09-29. Iliwekwa mnamo 2010-01-17.
  3. Mondomix, Julai 2003: Ted Josiah Archived 23 Machi 2009 at the Wayback Machine.
  4. GCAP Africa 17 Juni 2005: Major advertising campaign launched in Kenya Archived 2008-02-07 at Archive.today
  5. Daily Nation, Weekend Magazine, 30 Oktoba 2008: A new Kenyan sound on the way Archived 23 Julai 2011 at the Wayback Machine.