Achieng Abura

Mwanamuziki wa Kenya

Achieng Abura ni mwanamuziki kutoka Kenya, ambaye huimba nyimbo za Afro-jazz, Afro-fusion na injili.

Albamu yake ya kwanza ilikuwa ya injili na ilikuwa inaitwa I Believe mnamo mwaka wa 1990. Albamu zake zilizofuata Way Over Yonder na Sulwe . Mnamo mwaka wa 2002, wakati aliamua kuanza kuimba nyimbo za Afro-jazz, alitoa albamu iliyokuwa inaitwa Maisha . Baadaye alitoa albamu ijulikanayo kama Spirit Of a Warrior . Albamu yake ya hivi karibuni, inayojulikana kama Dhahabu Yangu ilitolewa mnamo mwaka wa 2007 na kampuni ya Blu Zebra studio, inayomilikiwa na Tedd Yosia.

Abura alishinda Tuzo la Kora mwaka wa 2004 kwa kuwa mwanamuziki bora wa kike katika Afrika Mashariki, tuzo ambalo lilishindwa pia na Tsedenia Gebremarkos wa Uhabeshi mwaka huo huo. Yeye ni balozi wa UNDP wakujitolea. Amezitembelea nchi nyingi sana Ulaya , kwa mfano Uhispania.

Alikuwa mmoja wa wanamuziki wa kundi la The Divas of the Nile ambalo liliwashirikisha wanamuziki wanne wa kike wa Kenya. Wanamuziki wale wengine walikuwa na pamoja na Suzzana Owiyo, Mercy Myra na Princess Jully. Kundi hili liliimba katka tamasha ya Mundial mjini Tilburg, Uholanzi mwaka wa 2007.

Yeye ndiye aliyekuwa mwalimu mkuu katika shindano la Tusker Project Fame mwaka wa 2008 na 2009. Amefanya kampeni kwa ajili ya mwito wa dunia dhidi ya umaskini [1] Yeye ni miongoni mwa wasanii wa Kenya ambao wamfadhiliwa na Alliance Française katika mji mkuu wa Nairobi. Abura aliteuliwa katika jamii la majukumu ya kijamii katika tuzo za Kisima za mwaka wa 2008 .

Alizaliwa mjini Eldoret. Anamiliki shahada ya Falsafa na Masomo ya Mazingira. Ana mtoto mmoja.

Mwanamuziki wa Kenya,Abbi alikuwa mwanamuziki wa zamani wa nyuma au msaidizi wa Abura kabla ya kuwa muimbaji maarufu wa kibinafsi.

Marejeo hariri