Abdullah bin Uthman

Malai Abdullah bin Malai Othman (alifariki 30 Juni 2019) alikuwa raisi wa Jumuiya ya Kusimamia Masuala Yanayohusiana na Tawahudi katika Mafunzo, Elimu na Rasilimali (SMARTER) huko Brunei.

Wasifu

hariri

Malai Abdullah alisomea uuguzi baada ya kuhitimu Chuo cha Anthony Abell, Seria mwaka wa 1973. [1]

Kabla ya kuanzisha uhamasishaji wa masuala yanayohusiana na usonji kupitia Kituo cha SMARTER Brunei, ambacho hatimaye kilipanuka na kujumuisha vituo vingine viwili,charity shop, na bakery, alikua akifanya kazi serikalini chini ya Wizara ya Afya (MoH). Kuanzishwa Kituo cha SMARTER Brunei kulichochewa na mwanawe wa pekee mwenye tawahudi, na mmoja wa binti zake sasa anafanya kazi na shirika hilo baada ya kupokea mafunzo binafsi kutoka kwa baba yake Mnamo mwaka wa 2018, alikuwa miongoni mwa watu kumi kutoka kanda ya ASEAN waliopokea tuzo ya kiraia ya Padma Shri kutoka kwa Raisi wa India, Ram Nath Kovind, kwa kazi yake ya kuboresha hali ya watoto na watu wazima wenye tawahudi. [2] [3] [4]

Malai Abdullah alifariki tarehe 30 Juni 2019, akiwa na umri wa miaka 66, akiwa na mke wake kando yake. Wakati wa kifo chake, alikuwa na matatizo ya kupumua, ambayo baadaye yalithibitishwa na wahudumu wa matibabu katika Hospitali ya Raja Isteri Pengiran Anak Saleha (RIPAS). [5] Ameacha mke wake, binti wanne, mtoto mmoja wa kiume, na wajukuu 11. [6]

  •   Padma Shri (2018)

Marejeo

hariri
  1. "1973 Sinaran Penuntut" (PDF). aacclassof1970. 1973. Iliwekwa mnamo 2024-07-19.
  2. "SMARTER President receives Padma Shri Award | Borneo Bulletin Online" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-12-14.
  3. Guan, Tan Wee (2018-04-04). "Autism society chief receives India's renowned Padma award". Asia News Network (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-12-14.
  4. "High Commission of India, Brunei Darussalam : News". www.hcindiabrunei.gov.in. Iliwekwa mnamo 2018-12-14.
  5. "HIGH COMMISSION OF INDIA, BRUNEI DARUSSALAM" (PDF). 2019-07-01. Iliwekwa mnamo 2023-04-23.
  6. Faisal, Fadley. "SMARTER Brunei President passes away", Borneo Bulletin, 2019-07-01.