Brunei (jina rasmi niː برني دار السلام , Negara Brunei Darussalaam, yaaniː Taifa la Brunei, Nyumba ya Amani) ni usultani mdogo na nchi huru kaskazini mwa kisiwa cha Borneo huko Asia ya Kusini-Mashariki.

بروني دارالسلام
Negara Brunei Darussalam
Bendera ya Brunei Daressalam Nembo ya Brunei Daressalam
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Daima katika utumishi kwa msaada wa Mungu"  (translation)
Wimbo wa taifa: Allah Peliharakan Sultan
"Mungu ambariki Sultani"
Lokeshen ya Brunei Daressalam
Mji mkuu Bandar Seri Begawan
4°55′ N 114°55′ E
Mji mkubwa nchini Bandar Seri Begawan
Lugha rasmi Kimalay na Kiingereza
Serikali Ufalme
Hassanal Bolkiah
Uhuru kutoka Uingereza
Mwisho wa hali ya nchi lindwa

1 Januari 1984
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
5,765 km² (ya 170)
8.6
Idadi ya watu
 - 2018 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
442,400 (ya 168)
332,844
72.11/km² (ya 134)
Fedha Brunei ringgit (BND)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+8)
(UTC)
Intaneti TLD .bn
Kodi ya simu +6731

-

1 Also 080 from Malaysia.


Imepakana na majimbo ya Sarawak na Sabah ya Malaysia tu, ingawa sehemu kubwa ya kisiwa hicho inatawaliwa na Indonesia.

Mji mkuu ni Bandar Seri Begawan.

Mtawala wa nchi ni sultani Hassan al-Bolkiah. Anasemekana kuwa kati ya watu tajiri zaidi duniani kutokana na mapato ya mafuta ya petroli.

Historia Edit

Dola la Brunei lilistawi kuanzia mwaka 1368 hadi karne ya 17 likienea katika sehemu kubwa ya Borneo na hata visiwa vingine. Lilipokea Uislamu katika karne ya 15.

Baada ya kunyang'anywa maeneo mengi na Wazungu (Wahispania, Waholanzi na Waingereza), mwaka 1888 sultani aliomba ulinzi wa Uingereza ambao uliendelea hadi uhuru wa mwaka 1984.

Watu Edit

Wakazi wengi (66%) ni wa jamii ya Wamalay, 10% ni Wachina, 3.4% ni Waborneo asili, 2.3% ni Wahindi, 16.8% wana asili tofauti.

Lugha rasmi ni Kimalay, lakini Kiingereza pia kinatambuliwa na katiba ya nchi.

Dini rasmi ni Uislamu wa madhehebu ya Sunni ambayo inafuatwa na thuluthi mbili za wakazi, lakini wakazi wengine wanafuata dini za Ubuddha (13%), Ukristo (10%) na dini za jadi (2%). Asilimia 7 hawana dini maalumu.

Tazama pia Edit

Marejeo Edit

Viungo vya nje Edit

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Taarifa za jumla
Biashara
Utalii
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Brunei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.