Abner Vinícius

Mchezaji wa mpira wa miguu

Abner Vinícius da Silva Santos (anayejulikana kama Abner Vinícius au kwa urahisi zaidi Abner tu. Alizaliwa 27 Mei 2000) ni mwanasoka wa Brazil ambaye anacheza kama beki wa kushoto wa Athletico Paranaense.

Kazi hariri

Abner alianza kazi yake ya kucheza mpira katika ngazi ya vijana kwenye klabu ya nyumbani iliyofahamika kama Grêmio Prudente. Kisha alikuwa na kipindi kifupi katika klabu ya Mogi Mirim, kabla ya kujiunga na na klabu Ponte Preta mnamo 2017.[1] Alipandishwa kuitumikia timu ya wakubwa mnamo 2019 na akafanya mazoezi yake ya kwanza mnamo 16 Machi 2019, kwenye mechi ya Derby Campineiro dhidi ya klabu ya Guarani kwenye uwanja wa Campeonato Paulista 2019, ambayo Ponte Preta ilishinda 3-0, alifunga bao lake la kwanza la kitaaluma mnamo 25 Mei 2019, ambalo lilikuwa bao la tatu kwa Ponte katika ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya klabu ya Paraná kwenye mechi ya ligi.[2]

Marejeo hariri

  1. "Abner – ADM Esporte". web.archive.org. 2019-07-23. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-23. Iliwekwa mnamo 2021-11-25. 
  2. Hero99. "Lateral-esquerdo Abner é o novo reforço do Athletico Paranaense". Athletico Paranaense – Site Oficial (kwa pt-br). Iliwekwa mnamo 2021-11-25.