Abubakar Shaabani Abdallah
futa Abubakar Shaabani Abdallah kijana aliyezaliwa na kukulia katika kijiji cha Ndembezi, ni mtoto wa tano katika familia ya watoto wa Maalim Shaabani Abdallah.
Alisomea katika shule ya msingi Ndembezi na kuendelea na masomo yake ya sekondari katika shule ya sekondari ya Taqwa, katika jiji la Mwanza.
Alijiingiza katika masuala ya siasa na hatimaye mnamo mwaka 2000 kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Ndembezi. Mpaka sasa kijana huyu anaendelea kushikilia nafasi yake ambapo pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga.