Kundi la AccessKenya

(Elekezwa kutoka AccessKenya Group)

AccessKenya ni kampuni ya kuwasilisha huduma za mtandao ziko nchini Kenya. Ilianzishwa katika mwaka wa 1995 na ndugu Daudi na Jonathan Somen ili kuwa kampuni ya kuuza huduma za kiteknolojia kwa wateja wa kampuni zilizo ndani ya Kenya ikiwa sehemu ya kampuni ya Communications Solutions Limited. Katika mwaka wa 2000, jina la AccessKenya ndilo lilioanza kutumika baada ya ndugu hao kuona haja ya kuwasilisha huduma ya mtandao kwa kampuni.

Kwa mara ya kwanza,AccessKenya iliuzia raia hisa yao katika Soko la Hisa la Nairobi hapo mwishoni mwa Aprili 2007. AccessKenya ikawa kampuni ya kwanza ya sekta ya teknolojia na mawasiliano ya Kenya kuorodheshwa kwa Soko la Hisa la Nairobi Hisa zilizotolewa kuuzwa za kwanza zilikuwa milioni 80 kwa bei ya shilingi 10 za Kenya kwa kila hisa.

AccessKenya inaajiri zaidi ya watu 270 watu hasa katika makao makuu ya Nairobi na miji mingine mikubwa kama Mombasa,Kisumu, Nakuru na Eldoret.

Hivi sasa,iko na wauzaji kila pahali katika taifa hili ili kuhakikisha wateja nchini kote wamepata bidhaa na huduma za kampuni hii. Tangu Februari 2008,AccessKenya imepata kampuni 3000 kama wateja; wateja wa kibinafsi 1500 na biashara ndogondogo takriban 125 ambazo nyingi zipo katika miji mikubwa - Nairobi, Mombasa, Kisumu na Nakuru.

AccessKenya iko na makao makuu yake katika jengo la Museum Hill Centre, karibu na Jumba la Kumbukumbu la Nairobi, kando ya Barabara ya Museum, katika mji wa Nairobi.

Hapo mwaka wa 2007,Kundi la AccessKenya lilinunua OpenView Business Systems kwa madhumuni ya kuongeza bidhaa zake kwa idadi ya bidhaa zilizouzwa na AccessKenya.

Mwezi wa Februari 2009, AccessKenya iliendelea na upanuzi na ikanunua Satori Solutions ,kampuni ya wastani ya kuwasilisha huduma za mtandao na mawasiliano, ili kusaidia kuza mauzo ya huduma yao mpya ya "SoHo" iliyolenga biashara ndogondogo na nyumbani za watu.Mikakati yao ya kununua Saroti Solutions na kampuni myinginezo imewasaidia na kuwaletea mapato mengi na kuifanya kuwa kampuni inayoongoza katika sekta yake.

Mfumo wa kibiashara

hariri

Kundi linajumuisha AccessKenya(kampuni ya Kenya inayoongoza kwa huduma ya mtandao) , Broadband Access (BLUE)(mojawapo ya kampuni kubwa zinazohusishwa na data) na sasa Openview Business Systems,. Kundi sasa lina zaidi ya kampuni 2400 za Kenya zinazolipia huduma za mtandao za waya,inaajiri zaidi ya watu 275 na ina ofisi za Nairobi na Mombasa pamoja na uwakilishi katika Kisumu, Eldoret, Nakuru na Nyeri.

Kundi hili pia limemea kwa 75% kila mwaka, kwa miaka minne iliyopita. AccessKenya ina inashirikiana na kampuni mbalimbali,moja ikiwa ni Cisco,Motorola, Oracle, Net App Gold na IBM .

Bidhaa za AccessKenya:

hariri
  • Access@Home
  • Yello
  • Go
  • Broadband Max 2
  • Bundu

Pia inatoa huduma za kusimamia tovuti, za kutoa virusi vya tarakilishi, huduma za usimamizi na huduma mbalimbali za kompyuta.

Makampuni yaliyo ndani ya AccessKenya sasa walio na leseni ni nne haswa kutoka Tume ya Mawasiliano ya Kenya (CCK) zikiwa leseni za DCNO, ISP, PDNO, na Local Loop.

Katika mwaka wa 2008,AccessKenya ilipigiwa kura kuwa kampuni bora kabisa katika sekta yake nchini Kenya na Openview Business Systems ikapigiwa kura kuwa nafasi ya pili katika kampuni za kutatua shida za mawasiliano na kiteknolojia. Tuzo nyingine ni :

  • Tuzo ya COYA ya kampuni bora ya pili katika sekta ya SME
  • Tuzo nyingine mbili za COYA
  • Openview ni imethibitishwa na ISO
  • Openview ilishinda tuzo ya CSK ya kampuni ya kutoa suluhisho za kiteknolojia katika miaka ya 2005, 2006 na 2007.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri