Soko la Hisa la Nairobi

Soko la Hisa la Nairobi (NSE) ndilo soko kuu la kuuza na kununua Hisa nchini Kenya. Lilianza mwaka wa 1954 kama Soko la Hisa la Ng'ambo wakati Kenya ilikuwa bado chini ya Ukoloni wa Uingereza kwa ruhusa ya Soko la Hisa la London. NSE ni mwanachama wa Shirikisho la Masoko ya Hisa ya Afrika.

Taswira

hariri

Soko la Hisa la Nairobi ndilo la nne kwa ukubwa Afrika katika mtazamo wa idadi ya hisa zinazouzwa, na la tano katika Thamani ya Hisa zote kama asilimia ya Pato la Taifa.[1] Soko hili hufanya kazi kwa ushirikiano na Soko la Hisa la Uganda na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam, pamoja na kusajili hisa mbalimbali katika masoko yote matatu.

Soko hili lina vikao vya kabla kati ya 09:00-09:30 na vikao vya biashara ya kawaida kati ya 09:30-03:00 siku zote za wiki isipokuwa Jumamosi, Jumapili na sikukuu zinazotangazwa na Soko mapema.[2]

Ofisi na sakafu ya biashara za NSE ziko katika jumba la Nation Centre katika baraste ya Kimathi. Biashara hufanywa kupitia Electronic Trading System (ETS) ambayo ilikamilika mwaka wa 2006. Mtandao wa Wide Area Network (WAN) uliwekwa mwaka wa 2007 na hili lilitupilia mbali haja ya Kampuni za kuuza na kununulia Hisa kuwapeleka mawakala wao (wafanyabiashara) kwenye ukumbi wa biashara ili kuuza au kununua hisa. Kwa sasa, shughuli za kununua na kuuza hufanywa kutoka ofisi zao kupitia mtandao wa WAN. Hata hivyo, baadhi ya mawakala bado wanaweza kufanya biashara kutoka sakafu ya NSE.

Fahirisi mbili hutumiwa kwa kawaida kupima utendaji. Ile ya NSE 20-Share Index imetumiwa tangu mwaka wa 1964 na hupima utendaji wa kampuni 20 bora zilizo na msimamo mzuri kifedha na ambazo zimezidi kurejesha matokeo mazuri ya kifedha mfululizo. Zilizojumuishwa katika fahirisi hii ni Kampuni ya Sukari ya Mumias, Express Kenya, Rea Vipingo, Sasini Tea, CMC Holdings, Kenya Airways, Safaricom, Nation Media Group, Barclays Bank Kenya, Equity Bank, Kenya Commercial Bank, Standard Chartered Bank, Bamburi Cement, British American Tobacco, Kengen, Centum Investment Company, East African Breweries, EA Cables, Kenya Power & Lighting Company Ltd na Athi River Mining. Fahirisi hii haswa hulenga mabadiliko ya bei ya makampuni haya 20.

Mwaka wa 2008, NSE All Share Index (NASI) ilianzishwa kama fahirisi mbadala. Kipimo chake ni kiashiria cha utendaji wa soko kwa jumla. Fahirisi hii hujumuisha hisa zote zilizouzwa au kununuliwa kila siku. Hivyo basi mtazamo wake ni utendaji kwa ujumla wa thamani ya hisa zote katika soko badala ya mabadiliko ya bei ya Hisa chache teule.

Hata hivyo kuna fahirisi nyingine ya tatu; AIG 27 Index ambayo hulinganishwa mabadiliko ya bei ya hisa za makampuni 27 ambazo zimetambuliwa kama zilizo imara kiasi. Wazo la msingi la fahirisi hii inalingana na ile ya NSE 20-Share Index. Lakini ilhali ile ya AIG imebainishwa na kampuni ya AIG (kampuni ya huduma za kifedha na sehemu ya AIG Group), ile ya NSE 20-share Index ni ya Soko la Hisa la Nairobi.

Kampuni zilizosajilishwa

hariri

Kampuni zilizokuwa zimesajilishwa kufikia Agosti 2015:

Sekta ya kilimo

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
EGAD Eaagads Limited Kahawa
KUKZ Kakuzi Limited Kahawa, chai, tunda la passion, avocados, machungwa, nanasi
KAPC Kapchorua Tea Company Limited Majani chai
LIMT Limuru Chai Company Limited Majani chai
SASN Sasini Tea and Coffee Majani Chai, Kahawa
WTK Williamson Tea Kenya Limited Chai

Magari na Vifaa

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
G&G Car & General Kenya Magari, vifaa vya kilimo na uhandisi
MASH Marshalls East Africa Archived 2 Oktoba 2015 at the Wayback Machine. Magari
FIRE Sameer Africa Limited Gurudumu
Kifupisho Kampuni Vidokezo
BBK Barclays Bank of Kenya benki na uwekezaji
CFC CfC Stanbic Holdings benki na uwekezaji
DTK Diamond Trust Bank Group benki na uwekezaji
EQTY Equity Group Holdings Limited benki na uwekezaji. imesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda, Dar es salaam na Rwanda
HFCK Housing Finance Company of Kenya Mikopo ya nyumba
I&M I&M Holdings Limited benki na uwekezaji
KCB Kenya Commercial Bank Group benki & uwekezaji. imesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda, Dar es salaam na Rwanda
NBK National Bank of Kenya benki na uwekezaji
NIC NIC Bank Group benki na uwekezaji
SCBK Standard Chartered of Kenya benki na uwekezaji
COOP Cooperative Bank of Kenya Banking, finance

Huduma za kibiashara

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
XPRS Express Kenya Limited Uchukuzi
HBER Hutchings Biemer Limited Samani
KQ Kenya Airways Shirika la Safari za ndege la Kenya; limesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda na Dar es Salaam
LKL Longhorn Kenya Limited Uchapishaji
NMG Nation Media Group Magazeti, majarida,stesheni za redio na televisheni. Shirika la Safari za ndege la Kenya; limesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda, Rwanda na Dar es Salaam
SCAN Scangroup Utangazaji na utafutaji masoko
SGL Standard Group Limited Magazeti, majarida,stesheni za redio na televisheni
TPSE TPS Serena Huduma ya kuchangia Utalii; Hoteli na Maeneo ya Starehe
UCHM Maduka ya Uchumi Maduka; Uchumi limesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda, Rwanda na Dar es Salaam

Ujenzi na Muhimbili

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
ARM Athi River Mining saruji, mbolea, madini; kuchimba migodi na uundaji
BAMB Bamburi Cement Limited saruji
BERG Crown Berger (Kenya) rangi
CABL East African Cables Limited Nyaya za umeme
PORT East Africa Portland Cement Company saruji

Kawi na Mafuta

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
KEGN KenGen kizazi cha umeme
KENO KenolKobil mafuta ya petroli
KPLC Kenya Power and Lighting Company Usambazaji umeme, usambazaji na reja
TOTL Total Kenya Limited mafuta ya petroli
UMME Umeme Usambazaji umeme, usambazaji na reja. Limesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda[3]
Kifupisho Kampuni Vidokezo
BRIT British-American Investments Company Bima
CIC CIC Insurance Group Limited Bima
CFCI Liberty Kenya Holdings Limited Bima
JUB Jubilee Holdings Limited Bima na uwekezaji. Limesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda na Dar es Salaam.
KNRE Kenya Re-Insurance Corporation Bima
PAFR Pan Africa Insurance Holdings Limited Bima

Uwekezaji

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
ICDC Centum Investment Company Limited Uwekezaji
OCH Olympia Capital Holdings Ujenzi na vifaa vya ujenzi
TCL TransCentury Investments Uwekezaji

Huduma za uwekezaji

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
NSE Nairobi Securities Exchange Soko la hisa

Viwanda na Muhimbili

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
BAUM A Baumann and Company Vifaa vya ujenzi
BOC BOC Kenya Gesi za viwandani
BAT British American Tobacco Sigara
CARB Carbacid Investments Gesi za vinywaji (Carbon dioxide)
EABL East African Breweries Bia; imesajiliwa katika masoko ya Hisa ya Uganda na Dar es Salaam
EVRD Eveready East Africa Betri
ORCH Kenya Orchards Limited Vinywaji vya matunda (juisi)
MSC Kampuni ya Sukari ya Mumias mashamba na utengenezaji wa sukari
UNGA Unga Group kusaga unga

Mawasiliano na Teknolojia

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
SCOM Safaricom Simu ya rununu, Mtambo wa intanet

Sehemu ya kampuni ndogo

hariri
Kifupisho Kampuni Vidokezo
ADSS Atlas Development & Support Services Utafutaji wa mafuta na petroli. imesajiliwa katika masoko ya Hisa la London.
HAFR Home Afrika Ujenzi wa vyumba
FTGH Flame Tree Group Holdings Ltd Bidha vya nyumbani
KVL Kurwitu Ventures Uwekezaji wa Kiisilamu

Soko la Mapato yasiyobadilika

hariri

(FISMS)

Kifupisho Kampuni Vidokezo
-- Kenya Power Lighting Ltd 7% PREF usambazaji umeme, usambazaji na reja
-- Kenya Power Lighting Ltd 4% Preferred --

Viungo vya nje

hariri

Tazama Pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "NSE - 4th largest Exchange in Africa". millenniumit.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-03. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2006. {{cite web}}: Unknown parameter |dateformat= ignored (help)
  2. [2] ^ Masaa ya Soko, Soko la Hisa la Nairobi kupitia Wikinvest
  3. "UMEME To Crosslist On Nairobi Stock Exchange". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-08. Iliwekwa mnamo 2015-09-24.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Soko la Hisa la Nairobi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.