Addison Road
Addison Road ni bendi la kuimba nyimbo za Kikristo ya aina ya pop ama rock.Bendi hili lilipiga saini mkataba na INO Records hapo mwaka wa 2007 na likatoa albamu yao ya kwanza,Addison Road.Albamu hii ilitolewa mnamo Mechi 18,2008. Nyimbo zao "All That Matters" na "Sticking With You" zilikuwa nambari 9 na 15 kati ya nyimbo zilizochezwa sana katika chati ya gazeti ya R&R ya Kikristo katika mwaka wa 2008.
Addison Road | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Aina ya muziki | Nyimbo za kisasa za Kikristo |
Kazi yake | Wanamuziki |
Ala | Gitaa na Piano |
Miaka ya kazi | 2002 hadi sasa |
Studio | INO Records |
Tovuti | http://www.addisonroad.com/ |
Wanachama wa sasa | |
Jenny Simmons Ryan Gregg Ryan Simmons Travis Lawrence Jeff Sutton | |
Wanachama wa zamani | |
Josh Anzaldua (2003–2005) |
Historia
haririLilivyoundwa
haririJenny Chisolm alikutana na Ryan Simmons katika Chuo Kikuu cha Baylor Waco,Texas.Walianza kuandika nyimbo muda mfupi baada ya kikundi hicho kuanza kupata matamasha ya kuimbia. Ryan alicheza gitaa na Jenny ndiye aliyekuwa mwimbaji. Ikawa dhahiri kwamba walihitaji bendi kamili, hivyo basi wakaungana na marafiki wawili: Jay Henderson anayecheza ngoma na Ryan Gregg(rafiki wao kutoka kanisa) achezaye gitaa.Gregg aliungana nao ingawa alikuwa katika bendi jingine lililoitwa na Tribe America. Walirekodi nyimbo nne za majaribio wakiwa "bendi lao mpya la Jenny Chrisholm".
Wakijitegemea
haririHapo Januari 2001, bendi lilipata mtu wa kuwatayarishia nyimbo na kuzirekodi,Chuck Dennie[1] na wakatoa albamu yenye urefu ya kawaida. Albamu ya kwanza yao ya kurekodi wakijitegemea iliitwa Not What You Think. Baadaye, wakaongeza rafiki mwingine ,Travis Lawrence, kama mwanachama wa bendi. Katika mwaka wa 2002, Ryan na Jenny walifunga ndoa, wakahamia Dallas ili kuwa bendi kama kazi yao kamili. Hatimaye,walibadili jina lao kuwa Addison Road. Liliitwa hivyo baada ya mhandisi wao wa sauti na muziki alipojifungua na kupata mwana aliyeitwa Addison. Walipenda jina hilo Addison na wakaliongeza lile la "Road" bila sababu halisi.
Baadaye,mwaka huo, walitoa albamu yao ya pili (bado wakijitegemea) iliyoitwa Breaking Beautifully.[2] Walipata mchezaji ngoma mwingine na wakaanza kuongoza ibada ya kanisa la Richardson First Baptist,hii ikafuatwa na bendi hilo kucheza nyimbo zao mbele ya vijana 8,000 katika majira ya joto ya mwaka huo. Hii ikawa motisha kwao ya kutoa albamu ya Always Loved You EP,iliyotolewa Juni 2005.[3] Wao walitoa albamu yao ya mwisho mnamo Julai 2006,iliyoitwa Some Kind Of Spark.[4]
Hapo mwaka wa 2009,bendi hilo lilizuru katika ziara ya Rock and Worship Show wakiwa pamoja na Jeremy Camp, MercyMe, Hawk Nelson na Tenth Avenue North. Jenny Simmons alikuwa mja mzito na hii ikafanya bendi kuimba wimbo mmoja tu katika kila sherehe. Hapo tarehe 15 Aprili 2009, Jenny alizaa mtoto msichana mwenye afya katika mji wao wa Dallas,TX.
Addison Road katika studio
haririBaada ya bendi hili kujitegemea kwa miaka sita, Addison Road lilipiga saini mkataba na INO Records katika mwezi wa Agosti 2007.[5] [12] Albamu yao ya kwanza ya studio ,Addison Road ilitolewa 18 Machi na ikawa #182 katika chati ya Billboard 200.[6]
Wanachama
haririWanachama wa sasa
hariri- Jenny Simmons – Mwimbaji kiongozi
- Ryan Gregg – Mchezaji gitaa kiongozi, mwimbaji
- Ryan Simmons – mchezaji gitaa, mwimbaji,mchezaji piano
- Travis Lawrence – mchezaji gitaa, mwimbaji
- Jeff Sutton – mchezaji ngoma
Wanachama wa kitambo
hariri- Josh Anzaldua – mchezaji ngoma (2003–2004)
Diskografia
haririAlbamu
hariri- Breaking Beautifully (Extended Play) (Septemba 2003)[7]
- Always Loved You EP (EP) (Juni 2005)
- Some Kind of Spark (Julai 2006)
- Addison Road (INO Records) (Machi 2008)
Nyimbo
hariri- "All That Matters" – #1 ,28 Machi 2008,chati ya R&R [8] na ikawa #9 katika nyimbo zilizochezwa sana katika chati ya mwisho wa mwaka wa gazeti la R&R
- "Sticking with You" – #2 katika chati ya R&R katika wiki 17 Oktoba 2008[9] a ikawa #15 katika nyimbo zilizochezwa sana katika chati ya mwisho wa mwaka wa gazeti la R&R.
Marejeo
hariri- ↑ "Addison Road > Overview". Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-10-20.
- ↑ http://www.independentbands.com/cd/addisonroad/breakingbeautifully.html
- ↑ "Addison Road, "Always Loved You EP"". Jesus Freak Hideout. Iliwekwa mnamo 2009-04-09.
- ↑ "Addison Road, "Some Kind of Spark"". Jesus Freak Hideout.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|1=
(help) - ↑ Tony Cummings (2008-09-04). "Addison Road:". Cross Rhythms. Iliwekwa mnamo 2008-10-19.
- ↑ "Addison Road – Addison Road". Billboard. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|3=
(help) - ↑ Diskografia; Jesus Freak Hideout ; 10 Februari 2008
- ↑ R&R magazine chart kama ilivyoripotiwa katika gazeti la Weekend 22,5 Aprili 2008
- ↑ "Christian CHR National Airplay". R&R. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-14. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameters:|4=
na|5=
(help)
Viungo vya nje
hariri- Tovuti Rasmi
- Addison Road katika MySpace