Adelaida Semesi
Adelaida Kleti Semesi, pia Adelaide K. Semesi (1951 – 6 Februari 2001),[1] alikuwa mtaalamu wa ikolojia kutoka nchini Tanzania. Adelaida alipata kuwa Profesa wa Viumbe Bahari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ambapo alijikita zaidi katika ekolojia ya mikoko. Sifa kubwa ya Semesi ni kuwa mwanamke wa kwanza kuwa profesa katika uwanja wa sayansi asilia nchini Tanzania.
Elimu
haririSemesi alizaliwa mwaka 1951 huko Haubi, Tanzania.[2] Alimaliza shahada ya kwanza ya Sayansi (BSc) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975,[2] na kisha kupata shahada ya uzamivu (PhD) kutoka taasisi hiyo hiyo mwaka 1979.[3]
Kazi
haririSemesi alianza kufundisha mwaka 1975 akiwa kama msaidizi. Akafikia hadhi ya uprofesa hadi alipofariki.[2] Mwaka wa1982, alianzisha mpango wa utafiti kuhusu ufugaji mwani huko Zanzibar; matokeo yake yalisababisha uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta hiyo, ambayo ilitoa ajira pana zaidi, hasa kwa wanawake.[2] Kazi yake kuhusu ekolojia ya mikoko ilianza mwaka 1990, na Tanzania ikawa moja ya nchi za mwanzo kuwa na mpango wa usimamizi wa mazingira kwa mikoko.[1] Pia alikuwa mtetezi wa maarifa ya kiasili yanayowasilishwa kwa njia ya mdomo. Alisisitiza zaidi matumizi yake ndani ya jamii, hasa yanayohusiana na nyanja za kilimo.[4]
Alipachikwa jina la "mama mikoko",[5][6] alibobea katika ekolojia ya mikoko,[5] alikuwa Mjumbe wa Baraza la Kimataifa la Ekolojia ya Mikoko,[1] Mjumbe wa Baraza la Jumuia ya Mikoko,[7] na mwanachama wa bodi ya wadhamini ya Western Indian Ocean Marine Science Association.[6]
Semesi alikuwa profesa wa kwanza mwanamke nchini Tanzania katika nyanja ya sayansi asilia.[6] Licha ya ubaguzi dhidi ya wanawake katika sayansi, alitambuliwa kwa wingi wa tuzo za kimataifa.[8] Tuzo hizo zilijumuisha ufadhili wa Fulbright katika Chuo Kikuu cha South Florida mwaka 1982, ambapo alifanya utafiti uitwao "Analysis of Certain Marine Phycocolloids".[9] Alipokea tuzo ya Pew Trust mwaka 1992, ambayo aliitumia kufanya utafiti mkubwa kuhusu eneo la Bagamoyo, ikijumuisha vyanzo vya baharini, takwimu za kijamii na kiuchumi na mambo mengine.[7]
Wakati wa kifo chake, Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[10] Alifariki tarehe 6 Februari 2001.[1] Kifo chake kilielezewa katika Pwani Yetu: The Newsletter of the Tanzania Coastal Management Partnership kama "hasara kubwa kwa uhifadhi wa mazingira ya bahari".[10]
Machapisho
hariri- Collen, J., M. Mtolera, K. Abrahamsson, A. Semesi and M. Pedersen. 1995. Farming and physiology of the red algae Eucheuma: Growing commercial importance in East Africa. Ambio 24(7): 497-450
- Mtolera, M.S.P., J. Collen and A.K. Semesi. 1995. Destructive hydrogen peroxide production in Eucheuma denticulatum (Rhodophyta) during stress caused by elevated pH, high light intensities and competition with other species. olera, M.S.P., J. Collen and A.K. Semesi. 1995. Destructive hydrogen peroxide production in Eucheuma denticulatum 30(4): 289
- Semesi A.K. 1993. Wetlands of sub-saharan Africa, their relevance and management. Proceedings of the conference on water and environment: Key to Africa's Development 151-164
- Engdahl, S., F. Mamboya, M. Mtolera, A. Semesi and M. Björk. 1998. The brown macroalgae Pakina boergesenii as an indicator of heavy metal contamination in the Zanzibar Channel. Ambio 27(8): 694-700
- Semesi, A.K. 1998. Coastal resources utilization and conservation issues in Bagamoyo, Tanzania. Ambio 27(8): 635-644
- Semesi, A.K. 1998. Mangrove management and utilization in Eastern Africa. Ambio 27(8): 620-626
- Mtolera, M.S.P., J. Collen and A.K. Semesi. 1996. Stressed-induced production of volatile halogenated organic compounds in Eucheuma denticulatum (Rhodophyta) caused by elevated pH and high light intensities. European Journal of Phycology 31(1): 91
- Bjork, M., S.M. Mohammed and A. Semesi. 1995. Coralline algae, important coral-reef builders threatened by pollution. Ambio 24(7): 502
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Adelaida Kleti Semesi 1951-2001" (PDF). Mangroves (24). International Society for Mangrove Ecosystems. Julai 2001.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 Oliveira, E. C.; Österlund, K.; Mtolera, M. S. P. (2003). Marine Plants of Tanzania. A field guide to the seaweeds and seagrasses of Tanzania (kwa Kiingereza). Sida/Department for Research Cooperation, SAREC. ku. Dedication.
- ↑ Nyika, E.A.; Ngusaru, A.S.; Mmochi, A. J. (2000). Directory of Marine Scientists Working in Tanzania (PDF). Tanzania Coastal Management Partnership.
- ↑ Brock-Utne, Birgit (1999). "African Universities and the African Heritage". International Review of Education. 45 (1): 87–104. Bibcode:1999IREdu..45...87B. doi:10.1023/A:1003577905270. ISSN 0020-8566. JSTOR 3444996. S2CID 142387251.
- ↑ 5.0 5.1 Brock-Utne, Birgit (8 Desemba 2022). Learning from and Teaching Africans (kwa Kiingereza). Cambridge Scholars Publishing. uk. 73. ISBN 978-1-5275-9157-8.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 6.2 "A Tribute to Adelaida K. Semesi" (PDF). WIOMSA Newsbrief. 6 (1). Machi 2001. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 22 Novemba 2021.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 "Adelaida Semesi". pew.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 4 Januari 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Masanja, Verdiana Grace (1 Oktoba 2010). Increasing Women's Participation in Science, Mathematics and Technology Education and Employment in Africa (PDF). United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO).
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Adelaida Semesi | Fulbright Scholar Program". fulbrightscholars.org. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 10.0 10.1 "Prof. Semesi's death, great loss to the nation and marine conservation" (PDF). Pwani Yetu: The Newsletter of the Tanzania Coastal Management Partnership (11). Machi 2001.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)