Adiós, Sabata
Adiós Sabata (Kiitalia: Indio Black, sai che ti dico: Sei un gran figlio di ..., kwa tafsri ya haraka unaweza sema "Indio Black, unajua ni nini nitakacho kwambia wewe... Wewe ni mtoto mkubwa wa ....") ni filamu ya Spaghetti Western iliyotolewa mwaka 1971 na iliongozwa na bwana Gianfranco Parolini.
Ni toleo la pili la mfululizo wa filamu za Sabata (kwa Kiing.. The Sabata Trilogy), ziliongozwa na mwongozaji mashuhuri bwana Gianfranco Parolini. Katika filamu hii Yul Brynner amechukua nafasi kutoka kwa mwigizaji wa awali bwana Lee Van Cleef, ambaye alicheza katika Sabata ya kwanza na ya tatu.
Hapo awali filamu ilibidi iyende kwa jina la Indio Black, lakini jina lilibadilishwa kutokana kwamba filamu ya kwanza ilifanya vizuri kwa jina la Sabata na ikaonekana kuwa na wapenzi wengi kuliko. Filamu hii ilibdi acheze Lee Van Cleef, lakini Cleef hakucheza kwasababu alikuwa anacheza filamu ya The Magnificent Seven Ride, humo alitumia jina lile lile la Chris Adams, ambalo Brynner alibebea umaarufu katika filamu ya awali ya The Magnificent Seven.
Njama
haririMuhtsari wa filmu
haririIlikuwa ndani ya nchi Mexiko iliyokuwa chini Dola la Maximilian I, Sabata alikodiwa na kiongozi wa guerilla bwana Señor Ocaño kwenda kuiba wagonload (Farasi mwenye kijumba nyuma) wa dhahabu kutoka mikononi mwa majeshi ya Kiaustrian. Sabata na rafiki zake wawili Escudo na Ballantine walifanikiwa kulitwaa wagon, lakini hawakukuta dhahabu bali waliukuta mchanga katika wagon hiyo, na dhabu ilikuwa ishachukuliwa na Amiri jeshi mkuu wa Kiaustria bwana Skimmel. Kwa hiyo Sabata akapanga mpango wa kurudisha dhahabu hizo.
Washiriki
hariri- Yul Brynner kama Sabata
- Dean Reed kama Ballantine
- Ignazio Spalla kama Escudo
- Gérard Herter kama Colonel Skimmel
- Sal Borgese kama Septiembre
- Franco Fantkamaia kama Señor Ocaño
- Joseph P. Persaud kama Hitano
- Andrea Scottia kama José
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Indio Black, sai che ti dico: Sei un gran figlio di... katika Internet Movie Database
- (Kiingereza) Adiós Sabata katika Allmovie