Adjudin
Adjudin (AF-2364) ni dawa ambayo inatengenezwa kwa ajili ya kuzuia uzalishaji wa manii kwenye korodani kwa mwanaume bila kuathiri uzalishaji wa homoni ya tesistosteroni. Ni dawa yenye asidi ambayo tafiti zake zinaendelea kufanyiwa kama inaweza kuwa njia ya uzazi wa mpango[1].
Adjudin ilikuwa katika hatua ya pili ya majaribio kwa binadamu mnamo 1 Mei 2007. Katika panya wa kiume inaonesha kupotea kwa seli za uzazi kutokana na kuvurugika kwa kazi ya kuunganisha seli za seritoli na seli za uzazi. Hudhoofisha muunganiko wa seli za seritoli na mbegu zinazokomaa ambayo inapelekea kupotea kwa mbegu.
Marejeo
hariri- ↑ Tash, Joseph S.; Attardi, Barbara; Hild, Sheri A.; Chakrasali, Ramappa; Jakkaraj, Sudhakar R.; Georg, Gunda I. (2008-06-01). "A Novel Potent Indazole Carboxylic Acid Derivative Blocks Spermatogenesis and Is Contraceptive in Rats after a Single Oral Dose1". Biology of Reproduction. 78 (6): 1127–1138. doi:10.1095/biolreprod.106.057810. ISSN 0006-3363.