Uzazi wa mpango
Uzazi wa mpango au uzazi wa majira maana yake ni njia mbalimbali ambazo binadamu analenga kuzuia wingi wa mimba ambao unadhaniwa kuweza kuleta madhara ya aina moja au nyingine.
Njia za zamani
haririNi hasa kumwaga shahawa nje ya tumbo la uzazi. Inashuhudiwa na Biblia (Mwa 38) kuhusu Onani, mwana wa Yuda (babu), aliyetaka kukwepa wajibu wa kuwazalia marehemu kaka zake. Ndiyo sababu alikufa.
Njia za teknolojia
haririBaadhi ya njia hizo za kuzuia uzazi ni: mipira ya kiume na ya kike na kufunga kizazi cha mwanamume au cha mwanamke: njia hizo haziui/kuharibu mimba, bali huzuia utungaji wenyewe wa mimba, lakini huwa zinaripotiwa kuwa na madhara kwa baadhi ya wanaozifuata, pia njia hizo zina asilimia tofauti za ufanisi. Zinaposhindikana, mtu aliyekusudia kukwepa mimba kwa mbinu yoyote anafikia kwa urahisi fulani uamuzi wa kuiua: hivyo hata njia hizo zinaweza zikaandaa mauaji ya halaiki za mimba, ambazo kwa baadhi ya watu ni binadamu tayari.
Wengine wanahesabu kama uzazi wa mpango hata tendo la makusudi la kuharibu mimba iliyokwishatungwa ambapo takribani mimba milioni mia na zaidi kila mwaka huharibiwa duniani. Zipo zinazoharibiwa na vidonge, sindano, poda, vitanzi[1] na vipandikizi, pengine bila ya wahusika kujua wala kutambua kilichotokea, kwa kuwa vifaa hivyo vinatangazwa kama njia za uzazi wa majira unaopanga upatikanaji wa mimba, kumbe ukweli ni kwamba vinaua mimba zilizokwishaumbwa, mbali ya kwamba vinaharibu afya ya akina mama.
Njia za sayansi zisizotumia teknolojia
haririPamoja na baadhi ya watu wengine, hasa wa dini mbalimbali, Kanisa Katoliki halikubali hata moja kati ya mbinu hizo, ila inaelekeza wale wanaohitaji kuairisha uzazi watumie ndoa siku zile ambazo mwanamke hawezi kupata mimba (yaani siku zote isipokuwa nne kwa mwezi, au zaidi ikiwa hana mwendo wa kawaida).
Njia hiyo ya asili haina madhara yoyote, wala haijengi hofu na chuki kwa mimba, wala haina gharama, hatimaye ina hakika kubwa (98-99% katika mtindo wa kupima ute wa uke uliovumbuliwa na bwana na bibi Billings). Njia hiyo inayofuata sayansi bila teknolojia inadai sadaka ya kujizuia kidogo, lakini uwajibikaji wa pamoja wa mume na mke unaohitajika unaweza kustawisha ushirikiano na uelewano kati yao.
Siku ambazo wanapumzika tendo la ndoa, upendo wao unaweza kujitokeza na kukua kwa njia tofauti (maongezi, matembezi na vitendo vidogovidogo vya mapenzi) bila kutegemea tendo la ndoa tu, kama kwamba ni dozi inayohitajika mara kwa mara.
Kinyume chake, njia za teknolojia zinategemea uamuzi hata wa mmojawao tu, zinajenga ubinafsi, zinamfanya mwanamume hasa azingatie kujamiiana tu hata mwanamke asiridhike na hivyo asipende kuungana na mumewe tena, zinaelekeza kutembea nje ya ndoa bila ya wasiwasi n.k.
Kwa hiyo njia hizo zinachangia sana kufanya ndoa zivunjike, watoto watelekezwe na nchi ziharibike, kama mang’amuzi yanavyoonyesha.
Bahati mbaya wanaozitegemea kwa kufaidika ni matajiri, nao wako tayari kutumia pesa nyingi ili kuzieneza hasa katika nchi maskini (k.mf. serikali ya Marekani na makampuni yake yanatafuta masoko mapya kwa biashara yao baada ya wateja wa nchi tajiri kuanza kung’amua madhara ya vifaa hivyo).
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- Moral Use of Natural Family Planning Archived 24 Februari 2014 at the Wayback Machine. (PDF). Prof. Janet E. Smith (Moral Theologian and Public Speaker). B.A., M.A., Ph.D., School of Theology, Fr. Michael J. McGivney Chair in Life Ethics, Professor of Moral Theology. At SHMS 2001–present.
Viungo vya nje
hariri- "Humanae Vitae". Encyclical of Pope Paul VI. The Holy See. Julai 25, 1968. Iliwekwa mnamo 2006-06-15.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Natural Family Planning katika Open Directory Project