Afya ya watoto na lishe barani Afrika

muhtasari kuhusu afya ya watoto na lishe katika Afrika

Afya ya watoto na lishe barani Afrika inahusika na utunzaji wa afya ya watoto hadi vijana katika nchi mbalimbali za Afrika. Haki ya kuwa na afya na lishe bora na ya kutosha inatambuliwa kimataifa kati ya haki za msingi za binadamu zinazolindwa na mikataba ya kimataifa, mikakati na matamko. Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) 1, 4, 5 na 6 yanaangazia, kwa mtiririko huo, jinsi afya ya mama, kutokomeza umaskini, njaa, vifo vya watoto, VVU / UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu na magonjwa mengine vilivyo muhimu katika muktadha wa afya ya watoto.[1]

Pamoja na ahadi hizi na maoni, ukweli ni kwamba vifo vingi vya watoto wadogo, haswa barani Afrika, vinaendelea kuwa sababu ya mashaka. Watoto waliozaliwa katika nchi zilizoendelea kama vile Uswisi wana hatari ya chini ya asilimia 1 ya kufa kabla ya umri wa mwaka 1, ambapo kwa watoto waliozaliwa katika nchi zinazoendelea, hatari iko karibu na asilimia 10 au zaidi. Ndani ya nchi zinazoendelea, kuna tofauti kubwa kati ya watu tajiri na maskini na wale wa mijini na vijijini.

Ulimwenguni kote, maendeleo makubwa yamepatikana katika juhudi za kupunguza vifo vya watoto. Idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 ulimwenguni imepungua kutoka karibu milioni 12 mnamo 1990 hadi milioni 6.9 mnamo 2011; na kiwango cha vifo cha watoto chini ya miaka mitano kimepungua kwa asilimia 41 tangu 1990 - kutoka vifo 87 kwa kila watoto 1,000 walio hai mnamo mwaka 1990 hadi 51 mnamo mwaka 2011. Sababu kuu za vifo kati ya watoto chini ya umri wa miaka 5 ni ugonjwa wa kisamayu (nimonia) asilimia 18, tatizo la mtoto kuzaliwa mapema (asilimia 14), kuhara (asilimia 11), changamoto wakati wa kuzaliwa (asilimia 9), na ugonjwa wa [Malaria (asilimia 7). Ulimwenguni kote, zaidi ya theluthi moja ya vifo vya chini ya miaka 5 vinatokana na upungufu wa lishe bora utapiamlo.

Marejeo hariri