Agaro
Agaro (au Haggaro) ni mji ambao unapatikana kusini mwa Ethiopia, jimbo la Oromia.
Barabara ambayo hapo awali iliunganisha Agaro na Jimma "ilijulikana zaidi kwa kina kuliko urefu wake" hadi maboresho yalipo kamilika mnamo mwaka 1962. Barabara ya Bedele, yenye urefu wa kilomita 96, ilikamilishwa mnamo 1968 kwa gharama ya dola milioni 12 (Ethiopia) ,na kampuni ya Ufaransa Razel Frères. Agaro ni moja ya vituo muhimu zaidi vya biashara ya kahawa nchini Ethiopia. Taasisi ya Jimma ya Afya ya Umma (sehemu ya Chuo Kikuu cha Jimma) ni kituo cha kufundishia huduma za afya huko Agaro.
Agaro ulikuwa ni mji mkuu wa Ufalme wa zamani wa Gomma,Gomma iliposhindwa na Dejazmach Besha Abuye mnamo mwaka 1886.Kufikia 1958,mji huu yalikuwa moja ya maeneo 27 nchini Ethiopia yaliyowekwa kama Jiji la daraja la kwanza.Fitawrari Gebre Kristos, alianzisha mashamba ya kahawa miaka ya 1950 kwenye ardhi aliyorithi kutoka kwa babu yake Fitawrari Wossen. Baada ya mapinduzi ya Ethiopia, Gebre Kristos aliacha shamba lake na kustaafu; shamba lake lilitaifishwa na Tangazo la Utaifishaji Ardhi la Machi 1975.mji huu una shule za sekondari na za msingi,pia una shule kongwe za sekondari na za msingi.
Idadi ya watu
haririSensa ya 1994 iliripoti mji huo ulikuwa na idadi ya watu 23,246 kati yao 11,687 walikuwa wanaume na 11,559 walikuwa wanawake.
Sensa ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2007, iliripoti jumla ya watu wote ni 25,458, kati yao 12,946 ni wanaume na 12,512 ni wanawake. Wakazi wengi walikuwa Waislamu, na asilimia 60.7 ya idadi ya watu waliripoti kwamba walifuata imani hiyo, wakati 33.76% ya idadi ya watu walikuwa Wakristo, na 5.04% walikuwa Waprotestanti.
Makadirio ya mwaka 2016 yalikuwa kwamba wakazi ni 39,174.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Agaro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |