Ahmad Tejan Kabbah
Alhaji Ahmad Tejan Kabbah (*16 Februari 1932) alikuwa rais wa Sierra Leone kuanzia 1996 hadi 1997 na kutoka 1998 hadi Septemba 2007.
Kabbah alifanya kazi miaka mingi katika Mradi wa Maendelo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kabla ya kurudi Sierra Leone. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe alingia katika siasa akachaguliwa kuwa rais mwaka 1996. Sehemu kuwa ya kipindi chake ilijaa mapambano na wanamgambo walioongozwa na Foday Sankoh.
Mwezi wa Mei 1997 Kabbah alipinduliwa na halmashauri ya kijeshi lakini kuingilia kati kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kulimrudisha madarakani kwa msaada wa kijeshi wa Nigeria hasa.
Mwaka 2002 hali ya vita vilimalizika na Kabbah akarudishwa katika uraisa katika uchaguzi wa mwaka huo.
Septemba 2007 kipindi chake cha pili kikaishi Kabbah akakabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi Ernest Bai Koroma