Airtel Tanzania
Airtel Tanzania Limited ni kampuni ya tatu kwa ukubwa ya mtandao wa simu nchini Tanzania, inayomilikiwa na Airtel Africa, ambayo ni tawi/kampuni tanzu ya Bharti Airtel ya India.
Kampuni hii iko nyuma ya Vodacom Tanzania na Tigo Tanzania. Kufikia mwezi Septemba 2017, Airtel Tanzania ilikuwa na wateja milioni 10.6 wa huduma za simu[1]. Hadi kufikia Desemba 2017, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Airtel Tanzania ilikuwa na asilimia 27.1 ya soko la simu za mkononi nchini Tanzania kwa idadi ya wateja, wakati huo ikikadiriwa kuwa na wateja milioni 10.86.[2]
Kampuni hii ni sehemu ya Airtel Africa, ambayo ni mtandao wa simu barani Afrika na ni mtoa huduma mkubwa katika bara la Afrika nje ya Afrika Kusini, ikifanya kazi katika nchi 14 za Afrika.[1][3]
Airtel Tanzania ilikuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano ya simu kuzindua huduma ya General Packet Radio Service/Enhanced Data Rates for GSM Evolution (GPRS/EDGE)[4] nchini Tanzania tarehe 3 Aprili 2006. Celtel Tanzania makao yake makuu yapo Celtel House, Dar es Salaam. Tarehe 1 Agosti 2008, Celtel ilibadilisha jina lake na kuwa Zain katika nchi zote za Afrika.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Airtel Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ 1.0 1.1 Amrit Raj, and Navadha Pandey (2 November 2018). "Tanzanian government disapproves of Airtel Africa IPO". New Delhi: Livemint.com. Retrieved 16 January 2019.
- ↑ Tanzaniainvest.com (8 February 2018). "The latest Quarterly Communications Statistics Report by the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) for the period October-December 2017". Dar es Salaam: Tanzaniainvest.com. Retrieved 16 January 2019.
- ↑ Team VCC (26 November 2018). "Airtel Africa hires JPMorgan, Citi, six other bankers for IPO". New Delhi: VCCircle.com. Retrieved 16 January 2019
- ↑ Celtel introduces first GPRS/EDGE service in Tanzania