Aisha Diori
Aisha Diori (alizaliwa 8 Septemba nchini Nigeria ) ni Mkurugenzi wa Matukio, Mhamasishaji wa Jamii juu ya VVU / UKIMWI na Kinga, mwalimu, Mtangazaji wa kipindi cha Maonyesho, Mshereheshaji Mwafrika, na amepewa jina la Mama wa utambulisho katika Utamaduni wa Mpira.[1][2] Baba yake ni Abdoulaye Hamani Diori, kiongozi wa kisiasa na mfanyabiashara wa Nigeria, ambapo mama yake anaitwa Betty Graves, mwanamke wa kwanza Mghana/Mnigeria kumiliki wakala wa kusafiri nchini Nigeria huko Afrika Magharibi.
Aisha Diori | |
Amezaliwa | 8 Septemba Nigeria |
---|---|
Nchi | Nigeria |
Kazi yake | Mhamasishaji |
Diori ana Shahada ya Uzamili ya Sanaa katika matangazo na mawasiliano ya masoko kutoka Taasisi ya Mitindo na Teknolojia ambapo alihitimu kwa point za juu sana magna cum laude. Kazi yake ya kuzuia na kupambana na VVU pamoja na vijana LGBTQ katika Utamaduni wa Mpira na tamaduni ndogo ya LGBT, imekuwa na ushawishi mkubwa katika uwanja wa afya ya umma.[3] Yeye ndiye mwanzilishi wa eneo la KiKi Ballroom[4]na anajulikana kama mjuzi na mtaalamu katika mahusiano ya kihistoria hasa katika eneo hili gumu la idadi ya watu.[5][6][7][8] Utaalam wake unaombwa kwa misaada na maendeleo ya mpango/programu,[9][10][11] na utafiti na maendeleo ya mtaala. Diori alifanya kazi katika Hetrick-Martin Institute ambapo alikua ni Mkurugenzi wa Afya na hali ya uzima,[12] na ndiye Mama wa Nyumba ya Iman, WBT (wanawake, kikundi cha wasagaji na waliobadilisha jinsia zao ama walio na mtazamo tofauti juu ya jinsia zao) katia nyumba za watu huko New York City.[13]Mnamo mwezi Februari 2014, Diori alijiunga na Kituo cha Utafiti wa Utamaduni wa watu Weusi huko Harlem kama Meneja wa Matukio Maalum, na kuendelea pia kuhusika na watu wa LGBTQ katika jamii ya mpira. Mnamo Agosti 2018, Diori alijiunga na MINA TV AFRICA katika NYC kama mwenyeji wa Tuzo lao na Kushinda Tuzo ya ABS inayoshughulikia habari zinazovuma katika Afrika na Ulimwenguni.
Maisha ya awali
haririAisha Dori alizaliwa wakati baba yake alikuwa uhamishoni[14] Ana kaka anayeitwa Chris, ambaye pia alizaliwa nchini Nigeria.
Diori alikuwa mfanyakazi wa kujitole kwa njia ya baraza la kanisa la jiji la New York. Alifanya mipango ya ndani ya jiji kwa watu wazima (wazee).
Marejeo
hariri- ↑ Ryan Joseph Photography, House and Ballroom Culture Photography. Ilihifadhiwa 24 Machi 2024 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Marlon Bailey, Constructing home and family: How the Ballroom community supports African American GLBTQ youth in the face of HIV/AIDS. Special Issue on LGBTQ people of color. Journal of Gay and Lesbian Social Services, 21, 171–188.
- ↑ The Institute For Gay Men's Health, AIDS Project of Los Angeles (APLA) and Gay Men's Health Crisis (GMHC), "What's Safe to you?" Safer Sex can mean different things to people. Archived 16 Septemba 2012 at the Wayback Machine
- ↑ See NYC's Ballroom Culture's History.
- ↑ Suze Myers, "Let's Have a Kiki: Drag Balls Still Thrive in Manhattan." Archived 13 Desemba 2012 at the Wayback Machine, the eye: the magazine of the columbia daily spectator, 2012.
- ↑ Marcus Brock of GLAAD, 'House-Mothers': Motherhood Redefined for LGBT Youth. Ebony.com, 11 May 2012.
- ↑ Ana Oliveira, GMHC 2004 Annual Report.
- ↑ Edgar Rivera Colón, Getting life in two worlds: power and prevention in the New York City House Ball community. Rutgers University, Electronic Theses and Dissertations, 2009.
- ↑ Centers for Disease Control and Prevention's Popular Opinion Leader (POL) A Community AIDS/HIV Risk Reduction Program for Gay Men Archived 9 Novemba 2013 at the Wayback Machine
- ↑ mPowerment Project, HIV prevention program that is designed to address the needs of young gay and bisexual men.
- ↑ "Centers for Disease Control and Prevention's AIDS Institute Individual- and Group-level HIV Prevention Interventions". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-13. Iliwekwa mnamo 2021-09-11.
- ↑ Hetrick-Martin Institute Staff, Aisha Diori. Archived 23 Julai 2012 at the Wayback Machine
- ↑ House of Iman past events.
- ↑ Chronology for Tuareg in Niger. Archived 18 Oktoba 2012 at the Wayback Machine Minorities at Risk Project, UNHCR Refworld, 2004.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aisha Diori kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |