Albamu (kutoka Kiingereza: album) ni kitabu chenye nafasi maalumu kwa ajili ya kuweka na kuhifadhi picha ndani yake.

Siku hizi albamu nyingi za picha na miziki zimo ndani ya sidii.

Pia ni jina la sahani maalumu ya santuri au sidii iliyohifadhi pamoja nyimbo kadhaa, au mkusanyo wa mambo yaliyorekodiwa na ambayo yanatolewa kwa pamoja.