Alclometasoni (Alclometasone), inayouzwa kwa jina la chapa Aclovate kati ya mengine, ni homoni za steroidi ambazo huzalishwa katika gamba la tezi la adrenali na hutumiwa kwa kawaida katika dawa ili kupunguza mwasho na kuzuia mwitikio wa mfumo wa kingamwili uliokithiri (corticosteroid) inayotumika kwa hali fulani za ugonjwa wa ngozi.[1] Hii ni pamoja na ni aina ya muda mrefu ya kuwasha kwa ngozi (atopic dermatitis), ugonjwa wa muda mrefu usioambukiza wa kingamwili unaojulikana na mabaka ya ngozi isiyo ya kawaida (psoriasis), na ugonjwa wa mzio wa ngozi unaotokana na mguso.[1] Dawa hii inatumika kwa ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na uwekundu, kuwasha, chunusi, kukonda kwa ngozi na alama za kunyoosha (striae).[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa Cushing na maambukizi. [1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii ni ya nguvu ya wastani.[2]

Alclometasoni iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1982 [1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Marekani, gramu 15 hugharimu takriban Dola 12 kufikia mwaka wa 2022.[3] Nchini Uingereza, gramu 50 hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £13.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Alclometasone Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1286. ISBN 978-0857114105.
  3. 3.0 3.1 "Alclometasone Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alclometasoni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.