Aleksandr Aleksandrovich Deyneka (kwa Kirusi: Алекса́ндр Алекса́ндрович Дейне́ка; Mei 20, 1899 – Juni 12, 1969) alikuwa mchoraji, msanii na mchongaji wa Umoja wa Kisovyeti. Anaonekana kama mmoja wa wachoraji wa karne ya 20 muhimu zaidi wa maumbo. Kazi zake ni mifano dhahiri ya uhalisia wa kisoshalisti[1].

Alexandr Deyneka

Deyneka yuko tamasha ya kupewa kwa tuzo za Lenin, Mei 1964
Amezaliwa Mei 20, 1899
Kursk, Milki ya Urusi
Nchi Umoja wa Kisovyeti
Amezikwa Kaburi la Novodevichiy, Moscow, Urusi
Anafahamika kwa Uchoraji·uchongaji·ualimu
Elimu VKhUTEMAS
Mtindo Uhalisia wa kisoshalisti
Mahusiano Serafima Lychyova (1930–1959), Yelena Volkova-Deyneka (1959–1969)
Tuzo Shujaa wa kazi ya kisoshalisti

Wasifu na maendeleo ya kazi

hariri

Amezaliwa katika ukoo wa mfanyakazi wa reli.

Alipata elimu yake ya kwanza katika Chuo cha Kharkov cha uchoraji (1915—1917) akiwa mwanafunzi wa Lubimov na Pestrikov. Ujana wake uliathiriwa na matukio ya mapinduzi. Alikuwa mpiga foto wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai, alibunia maigizo ya tathmilia na magarimoshi ya kishawishi. Pia alikuwa akilinda Kursk ulipovamiwa na majeshi ya harakati nyeupe. Miaka ya 1919 — 1920 aliongoza chumba cha uchoraji cha idara ya kisiasa ya Kursk.

Baada ya huduma ya kijeshi alipelekwa Moskow kujifunza katika VKhUTEMAS, kitivo cha uchapishi (1920—1925)[2]. Masomo ya Favorsky na mikutano yake na Vladimir Mayakovsky zilimwathiri sana. Mtindo wake wa kipekee ulijionyesha katika maonyesho makubwa yake ya kwanza mwaka wa 1924, aliposhiriki pamoja na Goncharov na Pimenov («kundi la watatu»). Miaka hiyo alichora picha ya «Ulinzi wa Petrograd» (1928), picha ya kwanza ya kimonyumental ya kihistoria ya kisovieti.Mwaka wa 1926 alipata sura ya mtu wa enzi mpya akichora «Ujenzini kwa karakana mpya»[3]. Mwaka wa 1930 alichorea mabango menye rangi na utungo za kuvutia, kama «Tuboreshe Donbass kwa mitambo» na «Mwanamichezo wa kike».

Alitembea Marekani mwaka wa 1935 kwa mwaliko wa Jumba la makumbusho la kisaana la Philadelphia na Taasisi ya kimarekani-kirusi. Pale Marekani maonyesho binafsi ya Deyneka yamefanyika. Wakati wa matembezi yake alichora tarakibu nyingi za maisha ya wamarekani. Pale pale amealikwa na uhariri wa jarida la Vanity Fair awachoree kigubiko.

Mwaka wa 1942 alichora mfululizo wa picha tamthilia zenye kite. Picha ya «Kitongoji cha Moskow. Novemba 1941» ni ya kwanza ya mfululizo huu. Mwaka wa 1942 alichora picha ya «Ulinzi wa Sevastopol» yenye sadiri ya ushujaa. Mwaka wa 1944 alichora picha ya «Upanuzi» ya kichanya.

Picha zake muhimu za kipindi cha baada ya vita ni «Mbio za kupokezana» (1947), «Baharini. Wavuvi wa kike» (1056), «Moskow wa kivita», «Huko Sevastopol» (1959). Mosaiki zake za kipindi kile kile zinapamba ukumbi wa maigizo wa Chuo kikuu cha Moskow cha Serikali (MSU), ukumbi wa Jumba la Mikutano la Kremlin na stesheni za «Mayakovskaya» na «Novokuznetskaya» za metro ya Moskow.

Amekufa Juni 12, 1969 akiwa na umri wa miaka 70.

Utendaji ya kijamii na wadhifu

hariri

Alikuwa mshirika wa jumuya za kisaana: Jamii ya watumizi vyombo («ОСТ», 1925—1927) akiwa mmoja wa waanzishi, Kundi la Oktoba («Октябрь», 1928—1930), Chama cha wachoraji wa mapinduzi (1931—1932).

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Deyneka aliishi Moskow na alichora mabango ya kisiasa kwa ajili ya karakana ya mabango ya kijeshi ya TASS (Shirika la habari la Umoja wa Kisovyeti). Mwaka wa 1942 alifanya matembezi kwenye mstari wa mbele mjini Yukhnov pamoja na mchoraji Nissky.

Mwanachama wa CPSU tangu 1960, mwanaakademia ya Akademia ya saana ya Umoja wa Kisovyeti tangu 1947. Mshiriki mwanahabari wa akademia ya saana ya Jamkhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani (1964).

Deyneka yuko kiwango cha juu «1A - msanifu mashuhuri duniani» katika Ukadiriaji wa kuungana wa saana.[4]

Kazi zake

hariri

Vyeo na tuzo

hariri
  • Shujaa wa kazi ya kisoshalisti (1969)
  • Msanifu mheshimiwa wa RSFSR (1945)
  • Mchoraji wa Umma wa RSFSR (1959)
  • Mchoraji wa Umma wa Umoja wa Kisovyeti (1963)
  • Tuzo ya Lenin (1964) — kwa mfululizo wa mosaiki zake «Mlinzi mwekundu», «Mkama maziwa wa kike», «Asubuhi njema», «Wachezaji wa hockey».
  • Nishani za Lenin mbili (ikiwemo 1969)
  • Nishani ya Bendera nyekundu ya kazi
  • Medali «Kwa ajili ya kazi ya jitihada wakati wa Vita Kuu ya Kizalendo 1941—1945»
  • Medali «Kwa heshima ya maadhimisho ya miaka 800 ya Moskow»
  • Medali kubwa ya dhahabu ya Maonyesho ya Duniani mjini Paris (1937)
  • Medali ya dhahabu ya maonyesho ya Duniani mjini Brussels (1958)
  • Medali ya dhahabu ya Akademia ya Saana ya Umoja wa Kisovyeti (1961)

Kumbukumbu

hariri
  • Amezikwa kaburi la Novodevichiy mjini Moskow
  • Asteroidi Deineka imetajwa hwa heshima yake[5]
  • Jumba la michoro la mjini Kursk imetajwa kwa heshima yake
  • Wito kutoka picha yake ulitumika kwa ajili ya kutaja maonyesho ya saana ya uhalisia wa kishoshalisti katika Jumba la michoro la saana na ubunifu za kirusi mjini London, mwaka wa 2016[6]

Viungo vya Nje

hariri
  1. "Art Turning Left, Tate Liverpool, review". The Telegraph (kwa Kiingereza). 2013-11-08.
  2. "Художник недели: Александр Дейнека". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-02. Iliwekwa mnamo 2016-01-18.
  3. "Дейнека Александр Александрович". Большая российская энциклопедия (kwa Kirusi). 2023-09-07. Iliwekwa mnamo 2024-07-16.
  4. "Московский художник Дейнека Александр Александрович". Socialist Realism. Kiev club of collectors. (kwa Kirusi).
  5. http://ssd.jpl.nasa.gov/sbdb.cgi?sstr=9514
  6. https://www.theguardian.com/lifeandstyle/2016/jun/13/superwomen-soviet-art-women-work-build-dont-whine-revolution