Umoja wa Kisovyeti

Jimbo la Kikomunisti huko Eurasia kutoka 1922 hadi 1991

Umoja wa Kisovyeti (kwa Kirusi: Советский Союз, tamka: sovjetskii soyuz, kifupi cha: Umoja wa Jamhuri za Kisovyeti za Kijamii) ilikuwa nchi kubwa duniani kati ya 1922 hadi 1991. Mara nyingi illitwa pia "Urusi" lakini ilijumlisha Urusi pamoja na maeneo mengine yaliyotwaliwa na Urusi katika mwendo wa historia kabla ya kutokea kwa Umoja wa Kisovyeti yaliyoendelea kuwa nchi huru baadaye.

Bendera ya Umoja wa Kisovyeti
Faili:Kolkhoznitsa.jpg
Sanamu ya mfanyakazi wa kiwandani pamoja na mkulima wa kike mjini Moscow

Ilianzishwa katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 ikachukua nafasi ya Milki ya Urusi ya awali. Umoja wa Kisovyeti ulitawaliwa na chama cha kikomunisti. Wakomunisti waliamua kutawala Dola la Urusi la awali kwa muundo wa shirikisho wakaunda jamhuri mbalimbali kufuatana na mataifa ndani ya eneo hili kubwa.

Kikatiba jamhuri hizi zote zilikuwa nchi huria lakini hali halisi zilitawaliwa zote kutoka makao makuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Katiba ilipata umuhimu tangu 1989 wakati wa mwisho wa utawala wa Wakomunisti ambako jamhuri zote zilitafuta uhuru wao zikaachana na Umoja.

Mwaka 1991 jamhuri wanachama za mwisho Urusi, Belarus na Ukraine ziliamua kumaliza Umoja wa Kisovyeti.

Viongozi hariri

Makatibu Wakuu wa Chama cha Kikomunisti hariri

Jamhuri za Umoja wa Kisovyeti hariri

Jamhuri za Kisovyeti (zote zimekuwa nchi huria) hariri

 
Ramani ya jamhuri za Umoja wa Kisovyeti
  1. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiarmenia imekuwa Armenia
  2. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiazeri imekuwa Azerbaijan
  3. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kibelarus imekuwa Belarus
  4. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiestonia imekuwa Estonia
  5. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kigeorgia imekuwa Georgia
  6. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi imekuwa Kazakhstan
  7. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikirgizi imekuwa Kirgizia
  8. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kilatvia imekuwa Latvia
  9. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kilithuania imekuwa Lithuania
  10. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova imekuwa Moldova
  11. Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi imekuwa Urusi
  12. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kitajiki imekuwa Tajikistan
  13. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kizturkmeni imekuwa Turkmenistan
  14. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine imekuwa Ukraine
  15. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki imekuwa Uzbekistan
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umoja wa Kisovyeti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.