Alglukosidasi alfa

Alglukosidasi alfa (Alglucosidase alfa), inayouzwa kwa jina la chapa Myozyme miongoni mwa mengine, ni dawa ya kutibu ugonjwa wa Pompe (ugonjwa wa kuhifadhi glycogen aina ya II).[1] Dawa hii inatolewa kwa sindano ya taratibu kwenye mshipa.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na athari za mzio, homa, maumivu ya kichwa, jasho, kichefuchefu, uchovu na maumivu ya misuli.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis).[3] Ni kimeng'enya kinachochukua nafasi ya alpha-glucosidase inayokosekana.[4]

Alglukosidasi alfa iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 2006. [1][4] Nchini Uingereza, miligramu 50 hugharimu Huduma za Afya za Kitaifa (NHS) takriban £360 kufikia mwaka wa 2021.[2] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 900 za Marekani.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Alglucosidase Alfa Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1117. ISBN 978-0857114105.
  3. 3.0 3.1 "Lumizyme- alglucosidase alfa injection, powder, for solution". DailyMed. 22 Februari 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 14 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Myozyme". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Lumizyme Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alglukosidasi alfa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.