Kimeng'enya

Vimeng'enya (ing. enzyme) ni molekuli za pekee za kibiolojia zinazojengwa na mwili na kazi zao ni kuarakisha michakato cha kikemia mwilini. Mara nyingi ni protini. Kichocheo kinaharakisha mmenyuko wa kikemia. Kwa hiyo vimeng'enya vinasaidia kazi za mwilini kama mmeng'enyo wa chakula.

Modeli ya kimeng'enya kinachoitwa TIM

Mfano wake ni kimeng'enya cha amylasi kinachopatikana katika mate mdomoni. Kimeng'enya hiki kinavunja molekuli za wanga kuwa molekuli ndogo zaidi. Hizi molekuli ndogo zaidi zinaendedela kuvukwa tumboni lakini kazi ya tumbo imesharahisishwa kutokana na kimeng'enya katika mate.

Kuna pia vimeng'emya nje ya mmeng'enyo tumboni vina kazi kote mwilini ndani ya seli kwa mfano vinaendesha kunakiliwa kwa DNA wakati wa kuzaa.

Vimeng'enya vimepata kazi pia katika bioteknolojia. Hapo vinatengenezwa katika maabara au hata viwandani ama kwa kutumia bakteria za pekee au kwa kuiga mchakato wa bakteria kwa mbinu za kikemia.

Kwa mfano vimeng'enya vinatiwa katika sabuni ya kuosha nguo na kuharakisha kuondolewa kwa mafuta au damu.


Viungo vya NjeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimeng'enya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.