All Out of Love
"All Out of Love" ni muziki wa miondoko ya pop, uliotoka mwaka 1980. Ulifika katika nafasi ya pili katika chati ya muziki ya Marekani na kufika katika nafasi ya 11 katika chati ya muziki ya Uingereza. Wimbo huu unaonekana kuwa moja kati ya nyimbo nzuri zaidi za mapenzi, na kupata nafasi 92, katika orodha ya VHI ya nyimbo 100 za mapenzi
“All Out of Love” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Air Supply | |||||
Muundo | CD single | ||||
Aina | Pop | ||||
Studio | Arista, EMI | ||||
Mtunzi | Graham Russell Russell Hitchcock | ||||
Mwenendo wa single za Air Supply | |||||
|
Waliorudiwa
haririWimbo huu umesharudiwa na wanamuziki mbalimbali kama vile, kundi la The Cantopop la msanii Alan Tam waliuridia wimbo huu na kuupa jina la "小風波" ambao ulifanya vizuri katika soko la Tam la nchini Hong Kong mwaka 1981. Pia mwanamuziki Andru Donalds alitoa wimbo huu kama single na kufikisha katika nyimbo tano bora za barani Ulaya kwa mwaka 1999, na nchini Australia kundi la boy band Mercury4waliujumuisha wimbo huo katika albamu yao ya debut album mwaka , 2004.Pia kundi la nchini Marekani linaloimba muziki wa taratibu maarufu kama R &B linaloitwa Jagged Edge waliuimba wimbo huo kwa ajili ya kutumika katika filamu ya Jamie Foxx iloitwa Breakin' All the Rules ya mwaka (2004).
Kundi la muziki la Westlife Kutoka nchini Ireland walirekodi wimbo huo kwa kushirikiana na mwimbaji wa nchini Australia Delta Goodrem katika albamu yao ya mwaka 2006, iloitwa , The Love Album, na pia waliuimba pamoja katika tamasha la The X Factor. Toleo la Westlife lilifika hadi nafasi ya 31 katika chati ya Swedish singles chart kama digital download mwezi Februari 2007,lakini haukuwahi kutoka kama toleo la kibiashara katika soko lingine lolote
Baada ya kundi la Westlife kutoa wimbo huo, kundi lingingine la OTT pia walitoa wimbo huo nchini Mwao na kufuatia kufikisha wimbo huo hadi Uingereza. Pia wimbo huu umesharudiwa kuimbwa na kundi jingine la Enigma, na baadae na mwimbaji wa Kizungu Declan Galbraith. Mwimbaji mwingine aitwaye John Barrowman alijumuisha wimbo huu katika albamu yake ya mwaka 2007 iliyoitwa Another Side. Baadae mwanamuziki Cliff Richard pia alirudia wimbo huu katiak albamu yake ya mwaka 2007 iliyoitwa Love... The Album. Na pia Keira Green Alirekodi wimbo huu kwa dizaini ya kucheza, mwaka 2006, na kuweza kupata nafasi katika albamu nyingi za kucheza. Pia mwanamuziki mwingine aliyerudia wimbo huu alitokea nchini Canada anayeitwa Mary Zilba ambaye yeye alirekodi katika miondoko ya pop na kuweza kufanya vizuri katika chati ya muziki ya Canada ya nyimbo 40 bora kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili.
Mwezi Juni mwaka 2003, wimbo huu ulitumika katika kampeni ya matangazo ya mgahawa wa Denny tangu mwaka 2007. Pia msanii Todd Solondz katika filamu yake ya Happiness ya mwaka 1998, pia katika tamthilia ya South Park katika sehemu ya "Raisins", na katika tamthilia ya Office sehemu ya "Stress Relief". Pia wimbo huu ulitumika.
Wimbo huu pia umetumika katika filamu ya Van Wilder, iliyotoka mwaka 2002, ambapo mhusika aitwaye Ryan Reynolds ambapo anasema kuwa, "'Gwen Used Me For Her Story, Then Married an Ass Wipe... and Ran Over My Heart With a Big Metaphorical Truck.' Kwa asili ulichezwa na Air Suply wakati wa mazungumzo na msichana mdogo aliyechezwa na Sophia Bush.
Katika mwanzo wa vichekesho vya Old Dogs, Seth Green samaki akiiimba wimbo huu kwa sokwe, jambo la kuvutia ni kuwa, wote wawili yaani Van Wilder na Old Dogs waliongozwa na Walt Becker.
Orodha ya Nyimbo
haririAir Supply version:
- "All Out of Love" – 4.01
- "Here I Am" – 3.48
- "Every Woman in the World" – 3.32
Andru Donalds version:
- "All Out of Love" (Radio Edit) – 4:00
- "All Out of Love" (Dance Radio Mix) – 3:59
- "All Out of Love" (Slow Ambient Mix) – 4:18
- "All Out of Love" (Ambient Club Mix) – 6:23
Chati
haririAir Supply (1980) | Ulipata nafasi |
---|---|
US singles chart | 2 |
UK singles chart | 11 |
Andru Donalds (1999) | Peak position [1][2] |
Austrian singles chart | 3 |
German singles chart | 3 |
Switzerland singles chart | 3 |
Westlife featuring Delta Goodrem (2007) | Peak position[3] |
Swedish singles chart | 31 |
Viungo Vya Nje
haririMarejeo
hariri- ↑ Germany peak position Ilihifadhiwa 22 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine. Retrieved 10 Agosti 2007.
- ↑ Austrian and Switzerland peak positions Retrieved 10 Agosti 2007.
- ↑ Swedish Charts Retrieved 18 Julai 2007.