Alofoni ni istilahi ya kifonolojia. Hasa ni kibadala ya fonimu katika mazingira fulani.

Sifa za alofoni hariri

Ladefoged (1962) ametaja sifa tatu za alofoni:

  1. hazibadilisha maana ya neno bali kinachobadilika ni umbo la neno tu
  2. hutokea katika mazingira tofauti ya kifonetiki;
  3. hufanana sana kifonetiki.

Mfano wa alofoni zinazotokea katika mazingira mbalimbali kifonetiki:

  • [t]~sauti hii inatokea katika kiingereza ikiwa kipasuo kitakuwa katikati mwa neno kwa mfano star.
  • [th]~sauti hii ya mpumuo hutokea ikiwa vipasuo sighuna vitakuwa mwanzoni mwa neno la kiingereza kwa mfano tar.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alofoni kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.