Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia

Lango la Lugha

Lugha (Kar: لغة) ni utaratibu kwa ajili ya kuwasiliana kati ya binadamu au kati ya viumbe vyovyote venye akili.

Mwaka wa 2008 umetangazwa kuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa. Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu. Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalum na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.

Mara chache neno lugha linatumika kwa taratibu za kuwasiliana za wanyama. Lakini taratibu hizo ni tofauti sana: Katika lugha za wanyama, sauti moja ina maana moja tu. Lakini katika lugha za binadamu, sauti nyingi zinaunganishwa kutengeneza maneno, na maneno mengi yanaunganishwa kutengeneza sentensi.

Hivyo mnyama ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini tofauti anaweza "kusema" mambo ishirini tu. Kwa upande mwingine mtu ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini, anaweza kusema mambo zaidi ya millioni.

Lugha ya mwezi (2009)

Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya kiarabu inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki. Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati na misemo na mithali na mashairi na mafumbo na vitendawili na nyimbo. Nayo inatumika katika mashule kufundishia elimu mbali mbali za dini na dunia, na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hii, vikiwa vya hadithi au hekaya au riwaya

Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambako wafanya biashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hii ilikuwa Kiarabu.

Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasilaino yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.

Picha ya mwezi (Mei 2009)


Picha inayoonyesha saa ya Kiswahili - kutoka kwenye Kamusi Hai ya Kiswahili.

Language topic of the month (May 2009)

Did you know...

No higher resolution available. Anglospeak(800px)Countries.png‎ (799 × 370 pixels, file size: 68 KB, MIME type: image/png)

Makala za Lugha

Lugha za Dunia

Lugha za Afrika: Tamazight, Kichadi, Kikushi, Kikanuri, Kimaasai, Kisetswana, Kiswahili, Kiturkana, Kixhosa, Kiyoruba, Kizulu, zaidi...

Lugha za Amerika: Aleut, Kikaribi, Kicherokee, Kiiroquois, Kikootenai, Kimaya, Kinahuatl , Kivavajo, Kiquechu, Kisalishi, zaidi...

Lugha za Asia: Kiajemi, Kiarabu, Kibengali, Kichina, Kijapani, Kiebrania, Kihindi, Kikorea, Kimongolia, Kisanskrit, Kitamil, Kikannada, Kitibeti, Kithai, Kituruki, Kivietnamu zaidi...

Lugha za Austronesia: Austric, Fijian, Hawaiian, Javanese, Kimalagasy, Malay, Maori, Marshallese, Kisamoa, Tahitian, Kitagalog, Tongan, zaidi...

Lugha za Ulaya: Kicheki, Kidenmark, Kieuskara, Kifaransa, Kihispania,Kiholanzi, Kiingereza (book), Kiitalia, Kijerumani, Kileonese, Kinorwei, Kipoland, Kireno, Kiromania, Kirusi, Kislovakia, Kituruki, zaidi...

Lughaunde: Kiesperanto, Kiido, Kivolapük, zaidi...


Aina za Lugha

Krioli, Lahaja, Lugha ambishi bainishi, Lugha ambishi changamani, Lugha ambishi mchanganyo, Lugha asilia, Lugha azali, Lugha biashara, Lugha chotara, Lugha ishara, Lughamata, Lugha muundo gubi, Lugha sanifu, Lugha tenganishi, Lugha ya kimataifa, Lugha ya kuundwa, Lugha ya taifa, Mame-lugha, Pijini


Isimu (Lango, Book)

Elimumitindo, Fonetiki, Fonolojia, Isimu amali, Isimu fafanuzi, Isimu historia, Isimujamii, Isimu jumuishi, Isimu kokotozi, Isimu matumizi, Isimu nafsia, Lafudhi, Leksikolojia, Mofolojia, Onomasiolojia, Semantiki, Sintaksi, Ulumbi

Tazama pia: Orodha ya Wanaisimu


Mifumo ya uandikaji

Alfabeti: Alfabeti ya Kiarabu, Alfabeti ya Kicyrillic, Alfabeti ya Kiebrania, Alfabeti ya Kilatini, zaidi...

Mifumo mingine ya uandikaji: Abjad, Abugida, Braille, Hieroglyphics, Logogram, Syllabary, zaidi...

Tazama pia: Historia ya alfabeti

Jamii za Lugha


Purge server cache