Amikto (kutoka Kilatini "amictus", "vazi") ni kitambaa cheupe cha kitani chenye mikanda ambacho katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo makleri au watumishi wengine wanavaa kabla ya mavazi mengine ya ibada.

Amikto ilivyo.

Kwa asili inavaliwa kichwani kama helmeti, halafu inaachwa iangukie begani, lakini siku hizi wengi wanaivaa moja kwa moja shingoni hadi mgongoni.

Lengo ni hasa kufunika nguo za kiraia zisitokeze kutoka chini ya kanzu nyeupe (alba).

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amikto kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.