Kanzu (kwa Kiingereza: tunic) ni vazi la rangi nyeupe au nyingine ambayo tangu kale huvaliwa na wanaume na wanawake vilevile katika maeneo mengi, kama vile bonde la mto Indus na Ulaya, lakini siku hizi matumizi yake yamepungua. Katika ustaarabu wa Magharibi, sanasana imebaki katika dini, yaani utawa na liturujia.

Mfanyakazi wa Roma ya Kale akiwa amevaa kanzu.
Wanaume waliovaa kanzu katika arusi huko Kampala, Uganda.

Matumizi yake Afrika

hariri

Ndani ya Afrika kanzu huwa na urefu wa kufika kwenye kifundo cha mguu au kwenye sakafu. Hutumika kama vazi la kitaifa kwa Tanzania (ambapo hilo neno lilitumika kwa kubadilishana na kaftan) na vilevile kwa Komoro (ambapo huitwa/hutamkwa 'Kandu', pia kwa jina la thawb kama katika nchi za Kiarabu). Vazi hilo pia huvaliwa kwenye baadhi ya mikoa ya pwani ya Kenya. Wanaume wa Uganda hulichukulia kama nguo muhimu sana (Kanzu ni neno la Kiganda lenye asili ya Kiswahili ambalo humaanisha "robe" au "tunic").

Kanzu za Uganda

hariri

Kanzu za Uganda zilianzishwa na ufalme wa Buganda na wafanyabiashara Waarabu[1]. Ssuuna alikuwa Kabaka wa kwanza wa Buganda kuvaa kanzu. Baada ya Kabaka kulipitisha hilo vazi ikawa kawaida kuvaliwa na wanaume wa Buganda wote. Kanzu ilisambaa kutoka kwa Waganda kwenda makabila mengine ikawa desturi ya taifa ya wanaume [2], ingawa katika Jamhuri ya Uganda si vazi la kitaifa kama ilivyo kwa majirani Tanzania.

Kanzu za Tanzania

hariri

Kwa Tanzania, kanzu ilianzishwa na wafanyabiashara na wamisionari kutoka Oman ambao walifanya dawah. Kanzu kwa Tanzania ilikuwa ni kidhihirisho cha mavazi ya Waarabu. Asili ya kanzu ni kutokea hariri. Kwa leo, kutokana na vikwazo vya Kiislamu kwenye mavazi ya hariri, ikawa inatengenezwa kutumia polyester au sintetiki ya vitambaa vilivyotengenezwa kwa kufanana na hariri. Sifa za ukinzani wa kanzu za Tanzania ni pindo linaloning'inia kwenye kola[3]. Kwenye baadhi ya familia, pindo hilo huwekewa marashi na baadhi ya mafuta ya Kiafrika na Kiarabu kabla ya sherehe ya harusi. Kanzu mara nyingi huvaliwa na kofia maalumu.

Kanzu za Kenya

hariri

Kwa Kenya, kanzu za Tanzania huvaliwa na Waislamu wa makabila yote. Wakristo huvaa kanzu (kwa kiwango kidogo) kwa matukio yasiyo rasmi, kujumlisha na huduma za Kanisa, lakini shati la dashiki au shati la kitenge hutumika kama vazi la kawaida kwenye harusi za Wakristo. Zote jamii za madhehebu huvaa kofia, kofia ndogo na kanzu. Kwa Kenya, ni desturi ya wakuu wa makabila na maimam wa Kiislamu kuvaa mkia mweusi na kanzu wanapohudhuria matukio ya kawaida. Kenya ni ya kipekee kati ya mataifa ya Afrika kwa hilo kwa kuwa ni nchi pekee isiyo na tamaduni za kitaifa[4]. Kwa kweli wanaume wa Kenya huvaa suti za Ulaya au tuxedos kwenye harusi au matukio mengine. Wengine wameanza kuvaa nguo za Kinigeria ambazo huitwa Agbada[5]. Ndani ya Kenya, wabunge wanaume hutakiwa kuvaa mitindo ya Ulaya kwenye mikutano yao[6].

Afrika ya Magharibi

hariri

Ndani ya Afrika ya Magharibi, vivyo hivyo kwa wingi vazi hilo lilivaliwa kwa kiasi kikubwa na watu wa Sahelia. Hapo ni pamoja na kaftan na boubou (mara nyingi huvaliwa kwenye matukio ya kawaida).

Mavazi ya harusi

hariri

Kanzu ni vazi la asili la harusi kwa wanaume wa nchi za Maziwa Makuu ya Afrika. Kipindi cha kusherekea harusi bwana harusi kimila huvaa kanzu nyeupe na kofia. Ndani ya Tanzania na Kenya, bwana harusi huvaa mkia mweusi au mweupe juu ya kanzu[3]. Bwana harusi na wanaume wengine kwenye sherehe ya harusi huvaa kanzu na jaketi la suti. Ndani ya Uganda, bwana harusi huvaa jaketi la suti juu ya kanzu na vazi la mahali huwa ni gomesi.

Tanbihi

hariri
  1. "Ugandanlink - World Wide Uganda Community - "KANZU" A Traditional Costume". web.archive.org. 2010-08-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-18. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  2. http://www.websters-online-dictionary.org/ka/kanzu.html
  3. 3.0 3.1 "mzuri-kaja.or.tz". web.archive.org. 2009-07-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-04. Iliwekwa mnamo 2022-03-17.
  4. Kenya unveils first national dress (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2004-09-16, iliwekwa mnamo 2022-03-17
  5. Kenya MPs fight 'colonial' dress code (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2003-07-17, iliwekwa mnamo 2022-03-17
  6. What is an African dress code? (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2004-03-01, iliwekwa mnamo 2022-03-17

Marejeo

hariri
  • "Dress and Adornment." The New Encyclopædia Britannica. 15th edition. Volume 17. 1994.
  • Payne, Blanche: History of Costume from the Ancient Egyptians to the Twentieth Century, Harper & Row, 1965. No ISBN for this edition; ASIN B0006BMNFS