Ampicillin ni antibiotiki inayotumika kuzuia na kutibu idadi ya maambukizo ya bakteria, kama vile maambukizo ya njia ya upumuaji, maambukizi ya mfumo wa mkojo, uti wa mgongo, maambukizi ya njia ya chakula yanaosababishwa na bakteria aina ya Salmonella (salmonellosis), na maambukizi ya utando wa ndani wa moyo (endocarditis).[2] Inaweza pia kutumika kuzuia maambukizi ya bakteria wa streptococcus (streptococcal) ya kikundi B kwa watoto wachanga.[2] Inatumiwa kwa mdomo, kwa sindano kwenye misuli, au kwa njia ya mishipa.[2] Kama viua vijasumu vyote, haina ufanisi kwa matibabu ya maambukizo ya virusi.

Jina la (IUPAC)
(2S,5R,6R)-6-([(2R)-2-Amino-2-phenylacetyl]amino)-3,3-dimethyl-7-oxo-4-thia-1-azabicyclo[3.2.0]heptane-2-carboxylic acid
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Principen, mengineyo[1]
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a685002
Taarifa za leseni EMA:[[[:Kigezo:EMA-EPAR]] Link]US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito A(AU) B(US)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo, kwa mishipa, au kwa misuli
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili 62% ±17% (uzazi)
< 30–55% (kwa mdomo)
Kufunga kwa protini 15 hadi 25%
Kimetaboliki 12 hadi 50%
Nusu uhai Takriban saa moja
Utoaji wa uchafu 75 hadi 85% kwa figo
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Data ya kikemikali
Fomyula C16H19N3O4S 
 YesY(Hiki ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na upele, kichefuchefu na kuhara.[2] Haipaswi kutumiwa kwa watu ambao wana mzio wa penicillin.[2] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha Clostridium difficile colitis au anaphylaxis.[2] Ingawa inaweza kutumika kwa wale walio na matatizo ya figo, dozi inaweza kuhitajika kupunguzwa.[2] Matumizi yake wakati wa ujauzito na unyonyeshaji yanaonekana kuwa salama kwa ujumla.[2][3]

Ampicillin iligunduliwa mwaka wa 1958 na ilianza kufanyiwa biashara mwaka wa 1961.[4][5] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[6] Gharama yake ya jumla katika nchi zinazoendelea ilikuwa kati ya Dola za Marekani 0.13 na 1.20 kwa chupa ya myeyusho wa mishipani kufikia mwaka wa 2014.[7] Nchini Marekani, inapatikana kama dawa ya kawaida na gharama ya matibabu ya siku 10 ni takriban $13.[2]

Marejeo

hariri
  1. "Ampicillin - international drug names". Drugs.com. 30 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 2.8 "Ampicillin". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Ampicillin use while Breastfeeding". Machi 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Fischer, Janos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 490. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Desemba 2016.
  5. Ravina, Enrique (2011). The evolution of drug discovery : from traditional medicines to modern drugs (tol. la 1). Weinheim: Wiley-VCH. uk. 262. ISBN 9783527326693. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Agosti 2016.
  6. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
  7. "Ampicillin". International Drug Price Indicator Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Machi 2017. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)