Maambukizi ya njia za mkojo

Maambukizi ya njia za mkojo ni maambukizi ya bakteria katika njia za mkojo.

  • Yanapoathiri sehemu ya chini ya njia hizo, maambukizi hayo hujulikana kama sisititisi ndogo (maambukizi ya kibofu).
  • Yanapoathiri sehemu ya juu ya njia za mkojo, maambukizi hayo hujulikana kama pilonifritisi (maambukizi ya figo).
Maambukizi ya njia za mkojo
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuUrology Edit this on Wikidata
ICD-10N39.0
ICD-9599.0
DiseasesDB13657
MedlinePlus000521
eMedicineemerg/625 emerg/626
MeSHD014552

Dalili katika sehemu ya chini ya njia za mkojo ni pamoja na uchungu wakati wa kukojoa na aidha kukojoa kila mara au kuhisi haja ya kukojoa (au zote mbili).

Dalili za maambukizi ya figo huhusisha pia homa na maumivu ya fumbatio (mwanya wa fupanyonga). Katika wazee na watoto wachanga, dalili haziwi wazi kila wakati.

Kisababishi kikuu cha aina hizo mbili niEscherichia coli. Hata hivyo, katika matukio machache, bakteria wengineo, virusi au kuvu wanaweza kuwa ndivyo visababishi.

Maambukizi ya njia za mkojo huwatokea mara nyingi zaidi wanawake kuliko wanaume. Nusu ya idadi ya wanawake huambukizwa wakati fulani maishani mwao. Marudio hutokea mara nyingi. Vipengele visababishi vilivyo hatari ni pamoja na ngono na pia historia ya kifamilia. Maambukizi ya figo yanaweza kufuatia maambukizi ya kibofu, pia yanaweza kusababishwa na maambukizi ya damu.

Utambuzi katika wanawake wachanga wenye afya unaweza kutazamwa kwa msingi wa dalili pekee. Utambuzi unaweza kuwa mgumu kwa watu walio na dalili zisizo wazi kwani bakteria wanaweza kuwepo hata kama mtu huyu hana maambukizi. Katika matukio yenye matatizo au ikiwa matibabu hayajafaulu, uchunguzi wa vimelea katika mkojo wakati mwingine husaidia. Mtu aliye na maambukizi ya kila mara anaweza kutumia kipimo kidogo cha antibiotiki kama namna ya kuzuia.

Matukio madogo ya maambukizi katika njia za mkojo hutibiwa kwa urahisi kwa kutumia mfululizo wa antibiotiki. Hata hivyo usugu dhidi ya antibiotiki zinazotumika kutibu hali hii, unaendelea kuongezeka. Watu walio na matukio yenye matatizo, wakati mwingine hushurutika kutumia antibiotiki kwa muda mrefu zaidi au watumie antibiotiki zinazodungwa ndani ya misuli. Ikiwa dalili hazipungui baada ya siku mbili au tatu, mtu atahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi. Katika wanawake, maambukizi ya njia za mkojo ndiyo maambukizi yanayotokea mara nyingi zaidi katika aina zote za maambukizi ya bakteria. Asilimia kumi ya wanawake hupata maambukizi ya nia za mkojo kila mwaka.

Dalili na ishara

hariri
 
Mkojo unaweza kuwa na usaha (hali inayojulikana kama piuria) kama inavyoonekana katika mtu aliye na sepsisi kufuatia maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.

Maambukizi ya sehemu ya chini ya mfumo wa viungo vya mkojo pia hujulikana kama maambukizi ya kibofu. Dalili zinazotokea mara nyingi zaidi ni hisia za kuchomeka wakati wa kukojoa na kukojoa kila mara (au kuhisi kukojoa) bila mchozo wa uke na maumivu mengi.[1] Dalili hizi zinaweza kutofautiana kutoka dalili zisizo kali hadi dalili kali[2]. Katika wanawake wenye afya njema, dalili hizi hudumu kwa wastani siku sita. Baadhi ya watu huwa na maumivu juu ya mfupa wa kinene au kwenye maumivu ya kiuno. Watu walio na maambukizi katika sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo au pilonifritisi (maambukizi ya figo), wanaweza kuwa na maumivu ya fupanyonga, homa au kichefuchefu na kutapika. Dalili hizi huambatana na kikundi cha dalili za maambukizi ya upande wa chini cha mfumo wa viungo vya mkojo.[2] Mkojo huwa na damu mara nadra sana[3] au kuwa na piuria (usaha katika mkojo).[4]

Katika watoto

hariri

Katika watoto wachanga, dalili pekee ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanaweza kuwa homa. Mashirika mengi ya afya hupendekeza uchunguzi wa vimelea katika mkojo wakati watoto wa kike wa chini ya umri wa miaka miwili au wa kiume ambao hawajatahiriwa wa chini ya umri wa mwaka mmoja wanapopata homa. Watoto wachanga walio na maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo wakati mwingine hukumbwa na ugumu wa kula, kutapika, hulala sana au kuonyesha dalili za umanjano. Watoto wakubwa wanaweza kukumbwa na kutoweza kujizuia kukojoa kwa ghafla (kupoteza udhibiti wa kibofu).[5]

Katika wazee

hariri

Dalili za mfumo wa viungo vya mkojo zinakosekana mara nyingi katika uzee. Wakati mwingine, dalili pekee ufukunyungu (kutoweza kujizuia kukojoa), mabadiliko katika hali ya nafsi, au uchovu.[2] Dalili ya kwanza katika wazee ni sepsisi, ambayo ni maambukizi ya damu[3] Utambuzi unaweza kutatizika kwa sababu wazee wengi wana ufukunyungu au wana dimenshia wana (hali ulemavu wa akili).

Kisababishi

hariri

E. coli ndicho kisababishi cha asilimia 80–85 ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Staphylococcus saprophyticus ndicho kisababishi cha asilimia 5–10 ya matukio haya.[1] Kwa nadra sana, maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo husababishwa na maambukizi ya virusi au kuvu.[6] Visababishi vya kibakteria ni pamoja na: Klebsiella, Proteus, Pseudomonas, na Enterobacter. Visababishi vya kibakteria huwa havitokei mara nyingi na kwa kawaida huhusishwa na hali zisizo za kawaida za mfumo wa viungo vya mkojo au kuweka katheta kwenye mfumo wa viungo vya mkojo.[3] Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanayosababishwa naStaphylococcus aureus kwa kawaida hutokea kufuatia maambukizi yanayotokana na damu.[2]

Jinsia

hariri

Ngono husababisha asilimia 75–90 ya maambukizi ya kibofu katika wanawake wadogo wanaojihusisha na ngono sana. Hatari ya kuambukizwa huhusianishwa na idadi ya marudio ya ngono.[1] Huku maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yakitokea mara vyingi wakati wanawake wanapoolewa, tamko "sisititisi ya fungate" hutumika mara nyingi. Katika wanawake baada ya ukomo wa hedhi ngono haizidishi hatari ya kupata maambukizi hayo. Kinyume chake, matumizi ya spemisidi huongeza hatari ya maambukizi hayo.[1]

Wanawake hupata maambukizi mengi zaidi ya aina hiyo kwa sababu wana urethra fupi na iliyo karibu na kinyeo.[7] Huku kiwango cha estrojeni ya wanawake (homoni) kinaposhuka kufuatia ukomohedhi, hatari ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo hupanda kwa sababu ya kupoteza flora ya uke inayokinga bakteria njema ukeni.[7]

Katheta za mkojo

hariri

Katheta huongeza hatari ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Hatari ya bakteriuria (bakteria kwenye mkojo) ni asilimia 3 hadi 6 kila siku. Antibiotiki haifaulu kuzuia maambukizi.[7] Hatari ya maambukizi husika inaweza kupunguzwa kwa kutumia katheta inapohitajika, kwa kutumia ufundisanifu usio na bakteria kuingiza katheta na kuhakikisha kuwa katheta hii inavuta mkojo bila kuzibika. [8][9][10]

Nyingine

hariri

Maambukizi ya kibofu ni ya kawaida sana katika familia kadhaa. Sababu nyingine za hatari ni pamoja na kisukari,[1] kutotahiriwa, na kuwa na kibofu kinene mno.[2] Vipengele vinavyochangia matatizo havijulikani vyema. Vipengele hivi ni pamoja na matatizo hatarishi ya kianatomia (yanaohusiana na muundo wa kimwili), kiutumizi au kiumetaboli. Maambukizi tata ya mfumo wa viungo vya mkojo huwa magumu kutibiwa na huhitaji utathmini, matibabu na ufuatilizi wa kina zaidi. [11] Katika watoto, maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo huhusianishwa na mwendo usio wa kawaida wa mkojo kutoka katika kibofu hadi ureta au figo na kufungika kwa choo.[5]

Pathogenesisi

hariri

Bakteria inayosababisha maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo huingia kibofuni kupitika urethra. Hata hivyo, maambukizi yanaweza kuingia kupitia damu au limfu. Madaktari wanaamini kuwa bakteria hii huingia katika urethra kutoka matumboni. Wanawake wako katika hatari kuu zaidi kwa sababu ya maumbile ya viungo vyao vya ndani. Baada ya kuingia katika kibofu, bakteria zaE. Coli zina uwezo wa kujibandika katika pembezo mwa kibofu na kuunda bayofilamu (mpako wa vidubini) inayopinga mwitikio wa kingamwili.[3]

Idadi kubwa ya njia za kukinga hazijathibitishwa kubadili matokeo ya mara nyingi ya maabukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Njia hizi ni pamoja na tembe za kuzuia mimba au kondomu, kukojoa punde baada ya ngono, aina ya chupi iliyotumiwa, mbinu za usafi wa kibnafsi zinazotumika baada ya kukojoa au kukunya, au kama mtu kwa kawaida huoga kwa karai au mfereji.[1] Vilevile, hakuna ushahidi wa kutosheleza kyuonyesha kuwa kukawisha mkojo, kutumia kisodo na kuonya uke kwa maji mengi kunaweza kusababisha maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.[7]

Watu wanaoambukizwa mara kwa mara na pia kutumia spemisidi au kiwambo kama njia ya kuzuia mimba wanashauriwa kutumia mbinu zinginezo.[3] (Maji au kidonge cha) matunda ya kranberi yanaweza kupunguza matukio katika watu wanaoambukizwa mara kwa mara. Hata hivyo, kuzoea matunda ya kranberi kwa muda mrefu ni jambo linaloweza kupelekea matatizo.[12] Matatizoo ya tumbo na matumbo hutokea katika zaidi ya asilimia 30 ya watu wanaokunywa maji ya matunda ya kranberi au kutuia vidonge vyake.[13] Kufikia mwaka wa 2011, probiotoki zinazotumika ndani ya uke zinzhitaji utafiti zaidi ili kutambua iwapo zina manufaa.[3]

Matibabu kwa kutumia dawa

hariri

Kwa watu walio na maambukizi yanayojirudiarudia, matumizi ya antibiotiki kwa muda mrefu hunufaisha.[1] Dawa zinazotumika mara nyingi ni pamoja na nitrofurantoin na trimethoprim/sulfamethoxazole. Ikiwa maambukizi yanahusiana na ngono (kujamiana), baadhi ya wanawake hunufaika kwa kutumia antibiotiki baada ya ngono.[3] Kwa wanawake walio katika kipindi cha ukomohedhi, estrojini (aina ya homoni) ya kupakwa ukeni imetambulika kupunguza kurejea kwa maambukizi. Kinyume na malai ya kupakwa, utumizi wa estrojini ya ukeni kutokapesari haujanufaisha inapotumika kama kipimo cha kiwango cha chini cha antibiotiki.[14] Idadi fulani ya chajo zingali zikitengenezwa kufikia mwaka wa 2011.[3]

Katika watoto

hariri

Ushahidi kuwa antibiotiki zinazozuia hupunguza maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo katika watoto ni mdogo sana.[15] Katika visa adimu katika watu wasio na matatizo ya figo, maambukizi yanayorejea ya mfumo wa viungo vya mkojo husababisha mataizo ya figo. Matatizo haya hupelekea chini ya theluthi ya asilimia (asilimia 0.33) ya ugonjwa wa muda mrefu wa figo katika watu wazima.[16]

Utambuzi wa ugonjwa

hariri
 
Basilia (bakteria za umbo la vijiti, zilizoonyeshwa hapa kama nyeusi na za umbo la maharagwe) zilizoonyeshwa katikati ya seli nyeupe za damu zilizo kwenye sampuli ya mkojo. Mabadiliko haya yanaonyesha maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.

Katika visa visivyo hatari, uchunguzi wa kimaabara hauhitajiki na maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanaweza kutambuliwa kulingana na dalili pekee. Uchanganuzi wa mkojo (kupima mkojo) unaweza kutumika kubainisha utambuzi katika matukio tata, kuchunguza uwepo wa nitraiti za mkojo chembechembe nyeupe za damu (lukosaiti) au lukosaiti esterasi. Uchuguzi mwingine, uchunguzi wa mkojo kwa kutumia hadumini, huangazia uwepo waseli nyekundu za damu, chembechembe nyeupe za damu au bakteria. uchunguzi viini wa mkojo huchukuliwa kuwa chanya iwapo utaonyesha idadi ya koloni za bakteria ikiwa 3 vitengo vinavyounda koloni 10 au zaidi kwa kila mL ya kiumbe cha kawaida cha njia ya mkojo. Uchunguzi pia unaweza kutumika kupima kiwango cha usikivu wa antibayotiki na kusaidia kubaini aina ya tiba ya antibiotiki itakayotumika. Hata hivyo, wanawake wanaotambulika kuwa na maambukizi wanaweza kuboresha afya kwa kutumia matibabu ya antibiotiki[1] Dalili za maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo zinaweza kuwa hafifu katika watu wazee, kwa hivyo utambuzi unaweza kuwa mgumu bila kupata vipimo vya kutegemewa.

Uainishaji

hariri

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanayohusisha sehemu ya chini ya mfumo wa viungo vya mkojo hujulikana kama maambukizi ya kibofu. Maambukizi yanayohusisha sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo hujulikana kama pilonifritisi au maambukizi ya figo. Iwapo mkojo una bakteria nyingi lakini hakuna dalili, hali hii kujulikana kama bakteriuria.[2] . Iwapo maambukizi yanahusisha sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo, mgonjwa huyu ana kisukari tamu, ana mimba, ni mume au anaudhaifu wa kingamwili (kingamwili iliyodhoofika kufuatia ugonjwa mwingine), maambukizi haya huchukuliwa kama yaliyo na matatizo..[3] Watoto wanapokuwa na homa pia, maambukizi haya ya mfumo wa viungo vya mkojo huchukuliwa kuwa maambukizi ya sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo. [5]

Katika watoto

hariri

Ili kutambua maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo katika watoto, viini vunafaa kutambulika katika mkojo. Mara nyingi, uchafuzi husababisha changamoto hivyo kipeo cha CFU/mL 5  10 hutumika kuchukua sampuli ya kati ya "kitegeo safi", CFU/mL 4  10 hutumika kwa sampuli zilizotolewa kwa katheta, na CFU/mL 2  10 hutumika kwa mpumuo wa juu ya kinena (sampuli inayotolewa moja kwa moja kutoka ndani ya kibofu kwa kutumia sindano). The Shirika la Afya Duniani hushauri kwamba "mifuko ya mkojo" isitumiwe kuchukua sampuli kwa sababu ya kiwango cha juu cha uchafuzi wakati mkojo huo unapochunguzwa. Inapendekezwa kutumia katheta iwapo mgonjwa hawezi kutumia choo. Baadhi ya makundi ya kiafya kama vile Chuo cha Marekani cha Wanapidriatiki, hupendekeza picha za matibabu za figo na voiding sistorethrogramu ya kuvuta (kutazama urethra na kibofu cha mkojo kwa kutumia picha za moja kwa moja wanapokojoa) katika watoto wote walio na umri wa chini ya miaka 2 na wana maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Hata hivyo, kwa sababu kuna ukosefu wa matibabu mwafaka iwapo matatizo yatapatikana, makundi mengine kama vile Taasisi ya Kitaifa ya Fanaka ya Matibabu hushauri picha za kila mara kwa watoto wa umri wa chini ya miezi 6 au walio na matokeo ya uchunguzi yasiyo ya kawaida.[5]

Utambuzi tofautishi

hariri

Katika wanawake walio na sevisitisi (inflamesheni ya seviksi) au vajinitisi (inflamesheni ya uke) na wavulana walio na dalili za maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo, maambukizi yanaweza kuwa yamesababishwa na Chlamydia trachomatis auNeisseria gonorrheae [17][2] Vajinitisi pia inaweza kusababishwa na maambukizi ya chachu [18] sisititisi ya ndani ya maungo (uchungu wa muda mrefu wa ndani ya kibofu) inaweza kuwa kisababishi cha dalili za mara kwa mara za maambukizi ya viungo vya mfumo wa mkojo, lakini ambao sampuli za mkojo wao havionyeshi maambukizi baada ya uchunguzi, wala hawapati nafuu baada ya kupewa antibiotiki.

Matibabu

hariri

Fenasopiridini inaweza kutumika pamoja na antibiotiki ili kupunguza muwasho wa maambukizi ya kibofu.[19] Hata, fenasopiridini kwa sasa haitumiki kwa sababu za usalama wa kiafya, hasa hatari kuu ya methemoglobinemia (kiwango cha juu ya kawaida cha methemoglobini katika damu).[20] Asetaminofeni inaweza kutumika kutibu homa.[21]

Wanawake walio na maambukizi madogo na ya mara kwa mara ya viungo vya mfumo wa mkojo hunufaika kutokana na tiba ya kibinafsi; ufuatilizi wa kibinafsi utahitajika tu iwapo matibabu ya kwanza hayatafaulu. Wanawake wanaweza kupata maelekezo ya antibiotiki kutoka kwa wataalamu wa afya kwa kutumia simu ya mkononi.[1]

Yasiyo na matatizo

hariri

Maambukizi yasiyo na utata yanaweza kutambuliwa na kutibiwa kwa msingi wa dalili pekee. [1] antibiotiki za kumeza kama vile trimethoprim/sulfamethoxazole (TMP/SMX), cephalosporin, nitrofurantoin, au fluoroquinolone hufupisha sana muda anaochukua mgonjwa kupona. Matibabu haya yote ni mwafaka kwa kiwango sawa.[22] Matibabu ya siku 3 kwa kutumia trimethoprim, TMP/SMX, au fluorokwinoloni kwa kawaida hutosha. Nitrofurantoin huhitaji siku 5-7 .[1][23] Baada ya matibabu, mgonjwa hutarajiwa kupata nafuu baada ya saa 36. Takriban asilimia 50 ya watu watapata nafuu bila matibabu baada ya siku au wiki chache.[1] Jamii ya Magonjwa Sambazi ya Marekani haipendekezi fluorokwinoloni kutumika kama matibabu ya kwanza kwa sababu inakisiwa kuwa kuitumia sana kunaweza kupelekea ukinzani dhidi ya kikundi hiki cha matibabu, hivyo kupunguza manufaa yake.[23] Licha ya tahadhari hii, kuna ukinzani ambao umetokea dhidi ya matibabu haya yote ambapo unahusiana na matumizi yake ya wingi.[1] Katika baadhi ya mataifa, Trimethoprim pekee huchukuliwa kama sawa na TMP/SMX.[23] Watoto walio na maambukizi madogo ya viungo vya mfumo wa mkojo mara nyingi hunufaika na matibabu ya siku 3 ya antibiotiki.[24]

Pilonifritisi

hariri

Pilonifritisi (maambukizi ya figo) hutibiwa kwa kina zaidi kuliko maambukizi madogo ya kibofu kwa kutumia matibabu ya muda mrefu ya antibiotiki au antibiotiki za ndani ya misuli.[25] Siku saba za kutumia florokuinoloni aina ya ciprofloxacin kwa kawaida hutumika katika sehemu za kijiografia ambapo kima cha ukinzani ni chini ya asilimia 10. Iwapo kima cha ukinzani katika eneo ni zaidi ya asilimia 10, kipimo cha dawa ya kudungwa ndani ya misuli iitwayo ceftriaxone mara nyingi hupendekezwa. . Watu walio na dalili mbaya zaidi wakati mwingine hulazwa hospitalini ili kuendelea kupewa antibiotiki.[25] Iwapo dalili hazitapungua kufuatia siku mbili au tatu za matibabu, matatizo kama vile kufungana kwa njia ya mkojo kunakotokana namawe ya figo huchunguzwa.[25][2]

Epidemiolojia

hariri

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo mara nyingi huwa maambukizi ya bakteria katika wanawake. Maambukizi haya hutokea mara nyingi kati umri wa miaka 16 na 35 . Asilimia 10 ya wanawake hupata maambukizi kila mwaka; asilimia 60 huwa na maambukizi katika wakati fulani maishani mwao.[1][3] . Mara nyingi, maambukizi hujirudia, huku takriban nusu ya watu wakiambukizwa tena kabla ya mwaka kuisha. Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo hutokea mara nne zaidi katika wanawake kuliko wanaume.[3]Pilonifritisi (maambukizi ya figo) hutokea kwa upungufu wa kati ya mara 20–30. [1] Pilonifritisi ndicho kisababishi kikuu chamaambukizi yanayotoka hospitalini, huku yakichangia takriban asilimia 40 ya maambukizi yanayotoka hospitalini.[26] . Viwango vya dalili za kibakteria katika mkojo huongezeka kwa miaka kutoka asilimia 2 hadi 7 katika wanawake walio katika umri wa kuzaa, hadi hata asilimia 50 katika wanawake wazee zaidi walio katika mashirika ya utunzaji.[7] Viwango vya dalili za kibakteria katika mkojo wa wanaume wa umri wa zaidi ya miaka 75 ni katik ya asilimia 7 na 10.

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanaweza kuwadhuru asilimia 10 ya watu katika miaka yao ya utotoni.[3] Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo katika watoto ndiyo yanayopatikana mara nyingi zaidi katika wavulana wasio tahiri wa umri wa chini ya mwezi 3, wakifuatwa na wasichana wa umri wa chini ya mwaka 1.[5] Hata hivyo, takwimu katika watoto hutofautiana pakubwa. Katika kikundi cha watoto walio na homa, kati ya asilimia 2 na 20 yao wa umri wa kati ya kuzaliwa na miaka 2 walitambulika kuwa na maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. [5]

Jamii na tamaduni

hariri

Nchini Marekani, maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo huchangia takriban ziara milioni 7 na ziara milioni 1 za vitengo vya dharura na watu 100, 000 wanaolazwa hospitali kila mwaka.[3] Gharama ya maambukizi haya ni kubwa sana kulingana na wakati unaotumika na bei ya utunzaji wa kiafya. Gharama ya moja kwa moja ya matibabu inakadiriwa kuwa  bilioni 1.6 za Marekani.[26]

Historia

hariri

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo ya ekuwa yakielezwa tangu siku za kale. Maelezo ya kwanza kuwahi kuandikwa, ambayo yanapatikana katika Mafunjo ya Ebers, ni ya takriban 1550 BC.[27] Wamisri walieleza maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo kama "kutoa joto kutoka ndani ya kibofu"[28] Mitishambakufyonza damu, na kupumzika ndizo aina matibabu zilizotumika kufikia mwaka wa 1930, wakati antibiotiki zilipatikana.[27]

Katika ujauzito

hariri

Wanawake walio na maambukizi nya mfumo wa viungo vya mkojo wako katika hatari zaidi ya maambukizi ya fiigo Wakati wa ujauzito, viwango vya juu vyaprojesteroni (homoni) huongeza hatari ya upungufu ulaini wa ureta na kibofu. Ulaini wa misuli uliopungua hupelekea ongezeko la uwezekano wa kurudi kwa mkojo, ambapo mkojo hurudi kupitia ureta kuelekea katika figo. Wanawake wajawazito hawana ongezeko la hatari ya dalili bakteriuria, lakini iwapo bakteriuria zipo, wanawake wajawazito wana hatari ya asilimia 25-40 ya maambukizi ya figo.[7] Kwa hivyo, matibabu hupendekezwa iwapo utambuzi wa mkojo utaonyesha dalili ya maambukizi—hata kama dalili hazipo. Cephalexin aunitrofurantoin hutumika kwa kawaida kwa sababu matibabu haya kwa kijumla huchukiwa kuwa salama katika ujauzito[29] Maambukizi ya figo wakati wa ujauzito yanaweza kupelekeakuzaliwa kabla ya kupevuka au pri-eklampsia (hali yashinikizo la damu.Matatizo ya figo wakati wa ujauzito yanaweza kupelekea mitukutiko).[7]

Marejeo

hariri
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 Nicolle LE (2008). "Uncomplicated urinary tract infection in adults including uncomplicated pyelonephritis". Urol Clin North Am. 35 (1): 1–12, v. doi:10.1016/j.ucl.2007.09.004. PMID 18061019.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 Lane, DR (2011 Aug). "Diagnosis and management of urinary tract infection and pyelonephritis". Emergency medicine clinics of North America. 29 (3): 539–52. PMID 21782073. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 Salvatore, S (2011 Jun). "Urinary tract infections in wom". European journal of obstetrics, gynecology, and reproductive biology. 156 (2): 131–6. PMID 21349630. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  4. Arellano, Ronald S. Non-vascular interventional radiology of the abdomen. New York: Springer. uk. 67. ISBN 9781441977311.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 Bhat, RG (2011 Aug). "Pediatric urinary tract infections". Emergency medicine clinics of North America. 29 (3): 637–53. PMID 21782079. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  6. Amdekar, S (2011 Nov). "Probiotic therapy: immunomodulating approach toward urinary tract infection". Current microbiology. 63 (5): 484–90. PMID 21901556. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 7.6 Dielubanza, EJ (2011 Jan). "Urinary tract infections in women". The Medical clinics of North America. 95 (1): 27–41. PMID 21095409. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  8. Nicolle LE (2001). "The chronic indwelling catheter and urinary infection in long-term-care facility residents". Infect Control Hosp Epidemiol. 22 (5): 316–21. doi:10.1086/501908. PMID 11428445.
  9. Phipps S, Lim YN, McClinton S, Barry C, Rane A, N'Dow J (2006). Phipps, Simon (mhr.). "Cochrane Database of Systematic Reviews". Cochrane Database Syst Rev (2): CD004374. doi:10.1002/14651858.CD004374.pub2. PMID 16625600. {{cite journal}}: |chapter= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  10. Gould CV, Umscheid CA, Agarwal RK, Kuntz G, Pegues DA (2010). "Guideline for prevention of catheter-associated urinary tract infections 2009". Infect Control Hosp Epidemiol. 31 (4): 319–26. doi:10.1086/651091. PMID 20156062.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  11. Infectious Disease, Chapter Seven, Urinary Tract Infections from Infectious Disease Section of Microbiology and Immunology On-line. By Charles Bryan MD. University of South Carolina. This page last changed on Wednesday, April 27, 2011
  12. Jepson RG, Craig JC (2008). Jepson, Ruth G (mhr.). "Cochrane Database of Systematic Reviews". Cochrane Database Syst Rev (1): CD001321. doi:10.1002/14651858.CD001321.pub4. PMID 18253990. {{cite journal}}: |chapter= ignored (help)
  13. Rossi, R (2010 Sep). "Overview on cranberry and urinary tract infections in females". Journal of clinical gastroenterology. 44 Suppl 1: S61-2. PMID 20495471. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  14. Perrotta, C (2008-04-16). "Oestrogens for preventing recurrent urinary tract infection in postmenopausal women". Cochrane database of systematic reviews (Online) (2): CD005131. doi:10.1002/14651858.CD005131.pub2. PMID 18425910. {{cite journal}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  15. Dai, B; Liu, Y; Jia, J; Mei, C (2010). "Long-term antibiotics for the prevention of recurrent urinary tract infection in children: a systematic review and meta-analysis". Archives of disease in childhood. 95 (7): 499–508. doi:10.1136/adc.2009.173112. PMID 20457696.
  16. Salo, J (2011 Nov). "Childhood urinary tract infections as a cause of chronic kidney disease". Pediatrics. 128 (5): 840–7. PMID 21987701. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  17. Raynor, MC (2011 Jan). "Urinary infections in men". The Medical clinics of North America. 95 (1): 43–54. PMID 21095410. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  18. Leung, David Hui ; edited by Alexander. Approach to internal medicine : a resource book for clinical practice (tol. la 3rd ed.). New York: Springer. uk. 244. ISBN 9781441965042. {{cite book}}: |edition= has extra text (help); |first= has generic name (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  19. Gaines, KK (2004 Jun). "Phenazopyridine hydrochloride: the use and abuse of an old standby for UTI". Urologic nursing. 24 (3): 207–9. PMID 15311491. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  20. Aronson, edited by Jeffrey K. (2008). Meyler's side effects of analgesics and anti-inflammatory drugs. Amsterdam: Elsevier Science. uk. 219. ISBN 9780444532732. {{cite book}}: |first= has generic name (help)
  21. Glass, [edited by] Jill C. Cash, Cheryl A. Family practice guidelines (tol. la 2nd ed.). New York: Springer. uk. 271. ISBN 9780826118127. {{cite book}}: |edition= has extra text (help); |first= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  22. Zalmanovici Trestioreanu A, Green H, Paul M, Yaphe J, Leibovici L (2010). Zalmanovici Trestioreanu, Anca (mhr.). "Cochrane Database of Systematic Reviews". Cochrane Database Syst Rev. 10 (10): CD007182. doi:10.1002/14651858.CD007182.pub2. PMID 20927755. {{cite journal}}: |chapter= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  23. 23.0 23.1 23.2 Gupta, K (2011 Mar 1). "International clinical practice guidelines for the treatment of acute uncomplicated cystitis and pyelonephritis in women: A 2010 update by the Infectious Diseases Society of America and the European Society for Microbiology and Infectious Diseases". Clinical infectious diseases : an official publication of the Infectious Diseases Society of America. 52 (5): e103-20. PMID 21292654. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  24. "BestBets: Je, matibabu ya muda mfupi ni bira kuliko ya muda mrefu katika matibabu ya maambukizi ya ya viungo vya mfumo wa mkojo". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-14. Iliwekwa mnamo 2013-11-28.
  25. 25.0 25.1 25.2 Colgan, R (2011 Sep 1). "Diagnosis and treatment of acute pyelonephritis in women". American family physician. 84 (5): 519–26. PMID 21888302. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  26. 26.0 26.1 Brunner & Suddarth's textbook of medical-surgical nursing (tol. la 12th ed.). Philadelphia: Wolters Kluwer Health/Lippincott Williams & Wilkins. 2010. uk. 1359. ISBN 9780781785891. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  27. 27.0 27.1 Al-Achi, Antoine (2008). An introduction to botanical medicines : history, science, uses, and dangers. Westport, Conn.: Praeger Publishers. uk. 126. ISBN 9780313350092.
  28. Wilson...], [general ed.: Graham (1990). Topley and Wilson's Principles of bacteriology, virology and immunity : in 4 volumes (tol. la 8. ed.). London: Arnold. uk. 198. ISBN 0713145919. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  29. Guinto VT, De Guia B, Festin MR, Dowswell T (2010). Guinto, Valerie T (mhr.). "Cochrane Database of Systematic Reviews". Cochrane Database Syst Rev (9): CD007855. doi:10.1002/14651858.CD007855.pub2. PMID 20824868. {{cite journal}}: |chapter= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maambukizi ya njia za mkojo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.