Analog Pussy

Kikundi cha wanamuziki

Analog Pussy (kwa Kiyahudi: אנלוג פוסי‎ ‎) ni kundi la wanamuziki ambalo lilianzia huko Israel, na ambalo hivi sasa liko nchini Ujerumani. [1]

Analog Pussy wakitumbuiza mubashara nchini Austria

Historia

hariri

Jiga alizaliwa Yerusalemu. Akiwa na umri wa miaka 15 alijifunza kucheza gitaa la besi na kucheza katika bendi za punk. [2] Alinunua kinanda kwa dola 50 na kompyuta na akaanza kutengeneza muziki akiwa peke yake.

Jinno alizaliwa Montevideo, Uruguay na kuhamia Israeli pindi alivyokuwa mtoto. Katika ujana wake alijaribu muziki wa elektroniki na ambaapo alikuwa akiunganisha muziki wa vinanda tofauti tofauti na kutoa muziki. Wawili hao walikutana wakati Jiga alipoachana na punk na kupendezwa na muziki wa kielektroniki [3] na mwaka wa 1997 wakaunda Analog Pussy pamoja.

Jiga na Jinno walijenga studio kwenye sebule yao walipokuwa wanakaa na ambapo walitoa nyimbo zao za kwanza kipindi hicho. Walifanya muziki wao upatikane bila malipo kwenye mitandao na kupata msingi wa mashabiki wengi na wanao wafuatilia. Baadaye, waliposhika nafasi ya juu katika rekodi za MP3.com, muziki wao ulipakuliwa na kupatikana zaidi ya mara milioni moja. [4]

Mnamo 1999, wakirudi kutoka kwenye ziara yao ya kwanza ya Uropa, walitia saini na lebo ya Kijerumani ya Balloonia na kutoa albamu yao ya kwanza iitwayo "Psycho Bitch From Hell". [5]

Jiga na Jinno walihamia Ujerumani mwaka wa 2002 [6] na kuzindua lebo yao ya rekodi "AP Records", ambayo toleo lake la kwanza lilikuwa albamu yao ya pili, "Underground".

Katikati ya 2004 walitoa albamu yao ya tatu "Trance 'N Roll". Nyimbo hizo zina ala za moja kwa moja, rifu za gitaa la roki na sauti. [7]

Ala inayohusishwa zaidi na Analog Pussy ni gitaa la besi la manjano la BassLab, linalochezwa na Jiga.

Kuvunjika

hariri

Wawili hao walivunja uhusiano wao wa binafsi na wa muziki mnamo 2007. Jiga anaendelea kucheza muziki mubashara katika majukwaa ya muziki na kuachia miziki mipya kama Analog Pussy. [8]

Matoleo

hariri
  • MP3001 (1999)
  • Psycho Bitch from Hell (Rekodi za Balloonia 1999)
  • Underground (2001)
  • Vinyl Trax (2002)
  • Trance N Roll (2004)
  • Future The Remixes (2004)
  • Mister Clown (2012)
  • Alive(2012)
  • Creme de la Pussy (2013)

Marejeo

hariri
  1. Prato, Greg "[Analog Pussy katika Allmusic Trance N Roll Review]", Allmusic, Macrovision Corporation
  2. ARTISTdirect biography, Analog Pussy biography Archived 5 Julai 2017 at the Wayback Machine.
  3. "Isratrance Interview". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-14. Iliwekwa mnamo 2023-04-14.
  4. Lewis, Judith (2001) "Independent Music’s Right to Fight", LA Weekly, 14 June 2001
  5. Discogs Psycho Bitch from Hell",
  6. "Mandarin Interview". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-22. Iliwekwa mnamo 2013-01-19.
  7. Bottenberg, Rupert (2000) "It's the end of the world as we know it >> And Israeli trance duo Analog Pussy feel just fine", Montreal Mirror
  8. Analog Pussy official facebook biography