Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) , rasmi Dola la Israel, ni nchi iliyoko Magharibi mwa Asia. Iko katika eneo la Kusini mwa Levant katika Mashariki ya Kati; na inapakana na Lebanoni na Syria upande wa kaskazini, Ukingo wa Magharibi na Jordan upande wa mashariki, Ukanda wa Gaza na Misri upande wa kusini-magharibi, na Bahari ya Mediterranean upande wa magharibi. Israel pia ina pwani ndogo kwenye Bahari ya Shamu kwenye pointi yake ya kusini kabisa, na sehemu ya Bahari ya Chumvi inapatikana kando ya mipaka yake ya mashariki. Mji wake mkuu ni Yerusalemu, wakati Tel Aviv ni eneo kubwa la mijini na kituo cha kiuchumi cha nchi hiyo.

Israel
מדינת ישראל (Kiebrania)
دَوْلَةْ إِسْرَائِيل (Kiarabu)
Wimbo wa taifa: "Hatikvah"
Eneo la Israeli na Maeneo walioteka ya Palestina
Mji mkuu
na mkubwa
Jerusalem
Lugha rasmiKiebrania
Kabila (2025)73.5% Wayahudi
21.1% Waarabu
5.4% Wengine
SerikaliJamhuri ya Muungano wa Rais
 • Rais
Isaac Herzog
 • Waziri Mkuu
Benjamin Netanyahu
Uhuru kutoka Uingereza
 • Uhuru
14 Mei 1948
Eneo
 • Jumlakm2 20,770 km²
 • Maji (asilimia)2.71%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2025 10,009,800
 • Msongamano454/km²/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
 • Jumla $565.878 bilioni (ya 47)
 • Kwa kila mtu $55,847
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
 • Jumla $550.905 bilioni
 • Kwa kila mtu $54,370
HDI (2022)0.915
SarafuShekel Mpya ya Israeli (₪) ILS
Majira ya saaUTCIST (UTC+2)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+972
Jina la kikoa.il
Tanbihi:
Eneo jumla la Israeli pamoja na Golan Heights na Jerusalem ya Mashariki ni 22,072 km²

Historia

Nchi ya kisasa ilianzishwa tarehe 14 Mei 1948 lakini nyuma kuna historia ndefu, ambayo kwa sehemu muhimu inasimulia na Biblia kama kiini cha historia ya wokovu.

Mji mkuu umekuwa Yerusalemu tangu mwaka 1950 lakini nchi nyingi hazikubali kuwa hivyo kwa sababu hali yake kadiri ya Sheria ya kimataifa haieleweki.

Demografia

Takriban 74.9% za wakazi ni Wayahudi ambao wengi wao wanafuata dini ya Uyahudi, na 20.7 % ni Waarabu ambao wengi ni Waislamu (16%) lakini pia Wakristo (2% za raia wote: kati ya Wakristo hao karibu 80% ni Waarabu). Wahamiaji wengi wasiopata uraia ni Wakristo.

Lugha rasmi ni Kiebrania na Kiarabu. Lugha nyingine zinazotumika sana nyumbani ni Kirusi, Kifaransa na Kiamhari, mbali ya Kiingereza.

Tazama pia

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Israel kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.