Ardabil

Ardabil (pia Ardabīl na Ardebīl , Kiajemi na Kiazeri : اردبیل) ni mji wa kihistoria kaskazini-magharibi mwa Iran. Jina Ardabil linatokana na jina la Kiajemi cha kale "Artawila", likimaanisha mahali patakatifu. [1] Ardabil ni makao makuu wa Mkoa wa Ardabil . Katika sensa ya 2011, idadi ya wakazi ilikuwa 564,365 katika familia 156,324, Wakazi wengi ni Waazeri. [2] [3] Ardabil pia inajulikana kwa patakatifu na kaburi la Safî ad-Dîn na jina lake lilikuwa chanzo cha nasaba ya wafalme wa Safavi .

Ardabil ikitazamwa kutoka mlimani
Kaburi la Sheikh Safi

MarejeoEdit

  1. Iranian Provinces: Ardabil
  2. Ardabil. Looklex Encyclopaedia. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 2013-08-13.
  3. Ardabīl. Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2013-08-13.

Tovuti za NjeEdit