Encyclopedia Britannica

(Elekezwa kutoka Encyclopædia Britannica)

Encyclopædia Britannica ni kamusi elezo kubwa na moja kati ya kamusi elezo iliyo-maarufu zaidi. Inaandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Kamusi elezo hii huchapishwa na kampuni binafsi ya Encyclopaedia Britannica, Inc. Awali ilikuwa ikichapishwa kwenye karatasi tu, lakini hivi karibuni imepanuka na kuwa na dijiti, au matoleo ya kompyuta vilevile. Kamusi elezo hii imegawanyika katika vitabu vingi sana. Makala za kwenye vitabu zimepangwa kwa mtindo wa kialfabeti. Kumekuwa na matoleo yake ambayo ni kwa ajili ya watoto vilevile. Hii ni kamusi elezo kubwa sana ya kuchapishwa. Kamusi elezo iliyo-kubwa ziadi ni Wikipedia. Watu wengi huhesabia kwamba ni kamusi elezo bora, kwa sababu ipo sahihi na ina mambo mengi.

Toleo la 15 la Britannica. Toleo la awali lenye ufito wa kijani ni Propædia; matoleo yenye ufito mwekundu na ufito-mweusi ni Micropædia na Macropædia, kwa pamoja. Toleo tatu za mwisho ni za Kitabu cha Mwaka wa 2002 (yenye ufito mweusi) na matoleo makuu-mawili (yenye ufito wa buluu iliokoza).


Kamusi elezo hii awali ilikuwa ndogo sana, toleo la kwanza lilikuwa na vitabu vitatu na ilitolewa mnamo mwaka wa 1768. Polepole likawa kubwa zaidi. Toleo jipya, toleo la 15, sasa lina vitabu takriban 29, jumlisha vitabu viwili ambavyo ni faharasa. Pia imemjulisha kitabu cha ziada kiitwacho Propaedia, kwa ajili ya kuainisha ufahamu. Vitabu 29 vimeumba Macropaedia na Micropaedia. Macropædia ni kikubwa kuliko vingine, chenye makala yenye maelezo zaidi ambazo pia zaweza kuwa na kurasa 300, -metengenezwa kwa vitabu 17, wakati Micropædia ni kidogo ambacho kawaida huwa na makala fupi na maneno machache chini ya 750. Micropædia hutumika kwa ajili ya kutazama kwa haraka zaidi, lakini iwapo utahitaji habari zaidi basi inakubidi utumie Macropædia. Kila kitabu kimoja ni kikubwa sana, zaidi ya kurasa 1,000 kwa kitabu. Kuna vitabu vya mwaka. Kila mwaka, kitabu kimechapishwa kuhusu matukio ya mwaka huo.

Makala za kwenye Britannica ni kwa ajili ya watu wazima walio-elimika, si kwa ajili ya watoto, na imeandikwa na wahariri takriban 100 na wachangiaji wataalamu zaidi ya 4,000. Watu wengi hudhania ni kamusi elezo bora, lakini Wikipedia bado inabaki kuwa maarufu kwa kuwa matumizi yake ni bure. Britannica ni kamusi elezo ya kale kwa lugha ya Kiingereza mpaka sasa. Ilianza kuchapishwa kwa mara ya kwanza kunako mwaka kati ya 1768 na 1771 huko mjini Edinburgh, Uskoti na kukua kwa umaarufu mkubwa, ikiwa na toleo lake la tatu mnamo 1801 ikiwa imeongeza vitabu 21.

Ukubwa wa vitabu vya Britannica karibia vyote vinafanana kwa takriban miaka 70, ikiwa na maneno yapatayo milioni 40 ikiwa ni nusu ya mada zilizopo ndani ya vitabu vyenyewe. Kamusi elezo hii awali ilikuwa ikimilikiwa na Uingereza. Kwa sasa inamilikiwa na Marekani, lakini bado inaandikwa kwa Kiingereza cha Uingereza. Muda wa ziada, kamusi elezo hii imekuwa na kipindi kigumu cha upatikanaji wa fedha, kitu ambacho kamusi elezo nyingi huzikumba.

Historia

hariri

Britannica imekuwa ikimilikiwa na watu tofauti, ikiwa ni pamoja na wachapishaji wa Kiskoti A & C Black, Horace Everett Hooper, Sears Roebuck na William Benton. Encyclopædia Britannica, Inc. inamilikiwa na Jacqui Safra, bilionea mwigizaji wa Uswisi. Teknolojia ya habari imekuwa vyema zaidi hivi karibuni na imekuwa kamusi elezo ya kielektronikia zaidi kama vile Microsoft Encarta na Wikipedia zimefanya watu kuto nunua kamusi elezo za kuchapishwa tena.[1] Hata hivyo bado inaweza kusalia, Encyclopædia Britannica, Inc. inaendelea kuwaambia watu kwamba Britannica ni nzuri na ipo sahihi zaidi, wametengeneza kamusi elezo ya bei rahisi, na kutengeneza matoleo ya kielektroni kwenye CD-ROM, DVD na Tovuti. Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1930, kampuni pia imekuwa ikitafutia masoko ya kazi za faida ya haraka.[2]

Matoleo

hariri
Matoleo ya Encyclopedia Britannica
Toleo Mwaka Idadi ya vitabu ya toleo

1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
11.
12.
13.
14.
15.
16

1768-1771
1777-1784
1788-1797, 1801 sup.
1801-1809
1815
1820-1823, 1815-1824 sup.
1830-1842
1852-1860
1870-1890
1902-1903
1910-1911
1921-1922
1926
1929-1973
1974-1984
tangu 1996-2004

3
10
18 + 2 nyong.
20
20
20 + 2 nyong.
21
21 + index
24 + index
toleo la 9 + 9 nyong.
29
toleo la 11 + 3 nyong.
toleo la 11 + 6 nyong.
24
28
32

Toleo la 16 la 2004 lina makala 75,000 yenye maneno milioni 44. Vitabu vyake 32 zaweza kunununuliwa kwa USD 1,400 kwa umbo la karatasi. Zapatikana pia kwa bei nafuu kama CD au DVD na kusomewa kwa compyuta.

Marejeo

hariri
  1. Day, Peter (17 Desemba 1997). "Encyclopaedia Britannica changes to survive". BBC News. Iliwekwa mnamo 2007-03-27. Sales plummeted from 100,000 a year to just 20,000. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  2. "Encyclopædia". Encyclopædia Britannica (14th edition ed.). 1954.
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Encyclopedia Britannica kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.